Tetesi za usajili Simba leo
Habari za michezo

KUHUSU KUTUA SIMBA….MAROUF TCHAKEI AFUNGUKA DILI LILIVYOKUWA ….

admin January 16, 2024 12:54 am

MAMBO bado ya moto, kuhusiana na usajili, baada ya kuwepo kwa tetesi za kiungo wa Singida Fountain Gate, Marouf Tchakei kuhusishwa kutua Simba, mwenyewe amefunguka ishu nzima.

Tchakei amesema hashangazwi kuona taarifa hizo hasa kipindi cha usajili, alichosisitiza hajazungumza na timu yoyote anachofahamu ni mali ya Singida.

“Nimepewa likizo ya wiki moja, nipo mapumziko hivyo mambo ya usajili siwezi kuyazungumzia hayo nawaachia viongozi ndio wenye uhalali na hilo,”amesema.

Ameongeza “Nina mkataba wa mwaka mmoja na nusu, hivyo ni makosa kuanza kuzungumza na timu ndio maana nasema viongozi ndio wenye uwezo wa kulizungumzia jambo hilo.”

Kiungo huyo msimu huu ameifungia Singida, mabao matano kwenye Ligi Kuu.

YANGA WAIJIBU SIMBA KWA KISHINDO….WASHUSHA MASHINE HII YA KAZI KUTOKA ULAYA… SINGIDA WAIKAZIA SIMBA ISHU YA PHIRI NA MIQUISSONE….

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply