Home Habari za michezo AFCON 2023:- MUISRAEL WA ZAMBIA APANIA KUIFANYA KITU MBAYA TANZANIA…

AFCON 2023:- MUISRAEL WA ZAMBIA APANIA KUIFANYA KITU MBAYA TANZANIA…

Habari za Michezo leo

Kocha wa timu ya taifa ya Zambia, Avram Grant amesisitiza kwamba amedhamiria kumaliza hasira zote za kukosa ushindi katika mechi ya kwanza iliyoisha kwa sare ya 1-1 dhidi ya DR Congo kwa kuishukia kisawaswa Taifa Stars ya Tanzania.

Chipolopolo ilipoteza uongozi ilioupata kwa bao la kushtukiza lililofungwa na nyota wake Kings Kangwa pale Yoane Wissa alipoisawazishia DR Congo.

Lakini kocha Avram Grant, ambaye aliwahi kuifundisha Chelsea ya Ligi Kuu ya England, amesema hatapoteza muda kuhuzunika kwa matokeo ya mechi ya kwanza bali anapanga ushindi katika mechi ijayo ya Zambia ya Kundi F dhidi ya Taifa Stars itakayopigwa Jumapili hii.

“Kila mechi ni tofauti na ijayo itakuwa tofauti na hii,” Grant aliwaambia wanahabari baada ya mechi.

“Hakika tutakuja na mbinu ya kupata ushindi dhidi ya Tanzania.”

Kocha huyo raia wa Israeli, amekiri kwamba DR Congo ilistahili kupata pointi katika mechi hiyo baada ya kupambana kiume kabla ya muda wa mapumziko.

“Ilikuwa mechi ngumu sana kwa kila timu lakini DR Congo walikuwa bora zaidi yetu,” alikiri Grant.

“Tulitembeza mpira vyema, lakini ilikuwa ngumu kwa washambuliaji wetu dhidi ya mabeki wanye miili mikubwa na nguvu nyingi.”

Huu ulikuwa mchezo mwingine kwa mchezaji kutoka nje ya Tanzania anayetumikia Ligi Kuu Bara kuanza kwenye nchi yake baada ya Inonga Baka kupata nafasi kwenye kikosi cha Congo akicheza kama mlinzi wa kati.

SOMA NA HII  UONGOZI WA YANGA WAFUNGUKA UGUMU WA MECHI YA LEO DHIDI YA AZAM