Habari za Yanga leo
Habari za michezo

PAMOJA NA LIGI KUU KUSIMAMA…ZOUZOUA AENDELEA KUPEWA ‘MAUA YAKE’….

admin January 19, 2024 5:15 pm

Kiungo kutoka visiwani Zanzibar Awesu Awesu amesenma anavutiwa na kiwango cha Kiungo Mshambuliaji wa Young Africans, Pacome Zouzoua na amekuwa akimfuatilia kila timu yake inapocheza.

Awesu anayeitumikia KMC FC inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara amesema kuna vitu vingi amekuwa akijifunza kutoka kwa raia huyo wa lvory Coast ikiwemo namna ya kuichezesha timu na kufunga mabao.

“Ukweli kwa wachezaji wa kigeni hasa katika eneo la kiungo navutiwa sana na kiungo wa Young Africans, Pacome, jamaa anajua sana mpira nimekuwa namfuatilia kwa karibu na kuna vitu vingi naiga kutoka kwake,” amesema Awesu.

Kiungo huyo aliyecheza timu nyingi kwenye Ligi ya Tanzania Bara, amesema wapo wengine wanaomvutia akiwemo Maxi Nzengeli na Fabrice Ngoma wa Simba SC, lakini Pacome ndio mtu anayemvutia kwa kiasi kikubwa.

Kiungo huyo alijiunga na Young Africans msimu huu akitokea Asec Mimosas na tayari amefunga mabao saba katika michuano yote ambayo Young Africans inashiriki.

WAKATI ISHU YAKE NA SIMBA HAIJAPOA…CHAMA KAIBUKA NA HILI KUHUSU TAIFA STARS… HUKU SIMBA NA YANGA ZIKIJIVUTA VUTA…AZAM FC WAPIGA HATUA MOJA MBELE KWENYE HILI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply