Habari za Yanga leo
Habari za michezo

MASTAA WAPYA WAIBUA VITA YANGA….WACHEZAJI WALIOKUWEPO WAANZA KUONGEA…

admin January 22, 2024 6:27 pm

Majembe mapya yaliyoongezwa ndani ya kikosi cha Young Africans yameongeza ugumu wa namba katika kikosi hicho, jambo linalowafanya wachezaji wote kujituma kwa juhudi kupenya kikosi cha kwanza.

Chini ya Kocha Mkuu, Miguel Gamondi ndani ya kikosi cha Young Africans ni Augustine Okrah ambaye ni winga raia wa Ghana na Joseph Guede huyu ni mshambuliaji raia wa lvory Coast wameongezwa ndani ya kikosi hicho kwenye dirisha dogo.

Mshambuliaji mzawa, Clement Mzize amesema kuwa uwepo wa wachezaji wapya katika kikosi hicho unaongeza ushindani wa namba katika kikosi hicho.

“Kweli hatujawa uwanjani kwa muda wananchi wamekosa ile burudani nasi tunaamini tutarejea tukiwa imara. Kuna wachezaji wapya wameongezeka katika timu, hilo linaongeza ugumu wa namba.

“Ambacho tunakifanya ni kuendelea kupambana hasa kwenye uwanja wa mazoezi kufanya vizuri na tukipata nafasi malengo ni kufanya vizuri ili kupata ushindi kwenye mechi ambazo tutacheza.” Amesema Mzize

BIL 25 ZATENGWA KUMVUA YANGA UBINGWA WA NBC….MO DEWJI ATAJWA..ISHU NZIMA IKO HIVI…. KICHUYA TENA…..MASTAA SIMBA WAMKARIBISHA KIBABE….

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply