Habari za Michezo leo
Habari za michezo

KUELEKEA AFCON YA TZ, KENYA NA UGANDA….TFF WAITWA MEZANI KUYAJENGA ….

admin January 26, 2024 6:12 pm

Makamu wa Rais wa Kamati ya Olimpiki Tanzania ‘TOC’, Henry Tandau ameliita Shirikisho la Soka nchini ‘TFF’ mezani kuelekea maandalizi ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika ‘AFCON 2027’ itakayoandaliwa na Tanzania, Kenya na Uganda.

Safari ya timu ya soka ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kwenye mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika, Ivory Coast ilifikia tamati juzi Jumatano (Januari 24) baada ya kutoka sare ya bila ya kufungana na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na kushika mkia kwenye Kundi F ikiwa na pointi mbili.

Tandau akizungumza jijini Dar es salaam amesema fainali za Ivory Coast kwa Taifa Stars zimefikia tamati na muhimu kwa TFF kuona namna gani wanajiandaa kwa mashindano hayo ambayo Tanzania itaandaa kwa kushirikiana na Kenya na Uganda mwaka 2027.

“Sisi kama Kamati ya Olimpiki tuko tayari kushirikiana na TFF kama wadau muhimu kuelekea michuano ya Kombe la Fainali ya Mataifa ya Afrika ambayo Tanzania tutaandaa kwa kushirikiana na Kenya na Uganda mwaka 2027.

MWAKINYO:- KUNA WATU WANATAKA KUNIKWAMISHA….WANAMPIGIA SIMU MPINZANI… SLOT YENYE UHAKIKA WA KUTOA MPUNGA MREFU KWENYE MERIDIANBET CASINO NI HII HAPA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply