Home Habari za michezo SIKU MOJA BAADA YA KUTUA BONGO…..GAMONDI AMCHOMOA GUEDE YANGA….

SIKU MOJA BAADA YA KUTUA BONGO…..GAMONDI AMCHOMOA GUEDE YANGA….

Habari za Yanga leo

BAADA ya straika mpya wa Yanga, Joseph Guede kutua kambini kuungana na wenzake mazoezini, kocha mkuu wa timu hiyo, Miguel Gamondi aliamua kumchomoa kundini kisha kumpa programu maalumu.

Guede aliyeingia kikosini kupitia usajili wa dirisha dogo na amejiunga na timu hiyo kwa mara ya kwanza akitokea Ivory Coast.

Akizungumza  kwa njia ya simu, Gamondi alisema baada ya nyota huyo kufika wanataka kwanza kumuangalia juu ya utimamu wa mwili na hivyo kumtenga kwanza na wenzake ili kumpa programu binafsi wakiendelea kumsoma kabla ya kumjumuisha na wenzake baadaye.

Gamondi alisema wachezaji wengi walishaanza mazoezi kasoro wale waliokuwa katika timu za Taifa, hivyo wako mbali tofauti na hawa wageni.

“Hatua ya kwanza ni kuangalia utimamu wake wa mwili baada ya hapo atakuwa na programu binafsi, kwani sitaki kumuwahisha kwa kuwa muda wa kumpa maandalizi bora bado upo. Wenzake tayari wako mbali baada ya mazoezi ya wiki mbili, hivyo hiyo programu itamwezesha awe fiti zaidi na kumrudisha katika ubora wake,” alisema Gamondi.

Guede tayari ameshaanza mazoezi leo (jana) ya kukimbia mbio tofauti akiwa chini ya kocha wa viungo, Taibi Lagrouni, wakati wenzake wakiwa wanacheza mechi ya wenyewe kwa wenyewe asubuhi hiyo.

SOMA NA HII  AZIZ KI ATUMIKA KUNADI MCHEZO WA POLISI TZ NA YANGA...VIINGILIO MECHI YA LEO VYAPANDA BEI KISA YEYE...

1 COMMENT