Habari za Yanga leo
Habari za michezo

SIKU MOJA BAADA YA KUTUA BONGO…..GAMONDI AMCHOMOA GUEDE YANGA….

admin January 29, 2024 9:55 am

BAADA ya straika mpya wa Yanga, Joseph Guede kutua kambini kuungana na wenzake mazoezini, kocha mkuu wa timu hiyo, Miguel Gamondi aliamua kumchomoa kundini kisha kumpa programu maalumu.

Guede aliyeingia kikosini kupitia usajili wa dirisha dogo na amejiunga na timu hiyo kwa mara ya kwanza akitokea Ivory Coast.

Akizungumzaย  kwa njia ya simu, Gamondi alisema baada ya nyota huyo kufika wanataka kwanza kumuangalia juu ya utimamu wa mwili na hivyo kumtenga kwanza na wenzake ili kumpa programu binafsi wakiendelea kumsoma kabla ya kumjumuisha na wenzake baadaye.

Gamondi alisema wachezaji wengi walishaanza mazoezi kasoro wale waliokuwa katika timu za Taifa, hivyo wako mbali tofauti na hawa wageni.

โ€œHatua ya kwanza ni kuangalia utimamu wake wa mwili baada ya hapo atakuwa na programu binafsi, kwani sitaki kumuwahisha kwa kuwa muda wa kumpa maandalizi bora bado upo. Wenzake tayari wako mbali baada ya mazoezi ya wiki mbili, hivyo hiyo programu itamwezesha awe fiti zaidi na kumrudisha katika ubora wake,โ€ alisema Gamondi.

Guede tayari ameshaanza mazoezi leo (jana) ya kukimbia mbio tofauti akiwa chini ya kocha wa viungo, Taibi Lagrouni, wakati wenzake wakiwa wanacheza mechi ya wenyewe kwa wenyewe asubuhi hiyo.

KWA PICHA HILI TU…..JE YANGA NA SIMBA WATATOBOA KLABU BINGWA AFRIKA…? KUELEKEA MECHI YA KESHO…..YANGA KUWAKOSA MASTAA HAWA SABA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

One response to “SIKU MOJA BAADA YA KUTUA BONGO…..GAMONDI AMCHOMOA GUEDE YANGA….”

  1. Charles Maziku Mathew says:

    Mpo viizuri Kwa kutoa habari za uhakika

Leave a Reply