Home Habari za michezo BAADA YA KUGOTESHWA KWENYE MAPINDUZI CUP….GAMONDI AAPA KUFA NA HILI NDANI YA...

BAADA YA KUGOTESHWA KWENYE MAPINDUZI CUP….GAMONDI AAPA KUFA NA HILI NDANI YA YANGA…

Habari za Yanga leo

Kocha Mkuu wa Young Africans Miguel Angel Gamondi, amesema hesabu zake kubwa kwa sasa ni kufanya vizuri kwenye mashindano makubwa matatu ambayo wanashiriki baada ya Mapinduzi 2024 kugota mwisho.

Ipo wazi kuwa Young Africans iligotea hatua ya Robo Fainali Mapinduzi 2024 ubingwa ukibaki kwa mara nyingine mbele ya Mlandege waliupata ushindi wa bao 1-0 Simba SC kwenye mchezo wa fainali iliyochezwa Januari 13 – 2024.

Gamondi ameweka wazi kuwa vita nyingine uwanjani ya kusaka ushindi inaendelea kwenye Ligi Kuu Bara, Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’.

Akizungumza jijini Dar es salaam, Gamondi amesema kuwa kila mashindano ambayo wanashiriki ni muhimu kufanya vizuri na kikubwa ni kupata ushindi uwanjani.

“Kwenye mashindano ambayo tunashiriki ni muhimu kupata ushindi kwa kuwa kila mchezo tunahitaji kupata matokeo. Wachezaji wanalitambua hilo hivyo tunafanyia kazi makosa yaliyopita ili tuwe imara.

“Makosa yaliyopita tunafanyia kazi sehemu ya mazoezi hilo linatufanya tuzidi kuwa imara kwa kupunguza zaidi makosa kwenye mechi ambazo tutacheza na tunaamini kwamba tutazidi kuwa imara.” amesema Gamondi.

SOMA NA HII  PANGA LA AINA YAKE LANUKIA SIMBA....MASTAA WATAKAOPIGWA CHINI WATAJWA...