Home CAF HUU HAPA UTAJIRI WA MASHINDANO YA AFCON….TIMU ZA TAIFA KULAMBA MAMILIONI YA...

HUU HAPA UTAJIRI WA MASHINDANO YA AFCON….TIMU ZA TAIFA KULAMBA MAMILIONI YA PESA…

Habari za Michezo leo

MBALI ya wachezaji mbalimbali kukomalia michuano ya Mataifa ya Afrika kizalendo zaidi kwa ajili ya mataifa yao, sababu nyingine zinazofanya wachezaji waonyeshe hali ya kupambana sana huwa ni bonasi mbalimbali wanazoahidiwa.

Kwenye mashindano mbalimbali, serikali ama vyama vya soka huweka ahadi za zawadi ama pesa kwa wachezaji ili kuwafanya wapambane zaidi.

Kwenye mashindano ya AFCON pia hali iko hivyo na hadi sasa kuna mataifa ambayo tayari imesharipotiwa kwamba wameahidi mastaa wao pesa ikiwa watachukua ubingwa, kushinda mechi ama kufika hatua fulani.

Ukiondoa ahadi za timu, pia CAF nayo imeongeza pesa zaidi ambapo mwaka huu bingwa atapata maradufu. Hapa tumekubainishia mgawanyo wa pesa zote za zawadi za AFCON, ukilinganisha na mashindano mengine na pesa ambazo mataifa mbalimbali yameahidi kuwapa wachezaji wao ikiwa watafanya vizuri.

ZAWADI ZIPOJE

Kwa mujibu wa tovuti mbalimbali ikiwamo Goal.Com, CAF imeandaa jumla ya Dola 14.8 milioni zitakazotumika kama zawadi za fainali hizi.

Mwaka huu kuna ongezeko la Dola 2 milioni kutoka Dola 5 milioni ambazo ziligaiwa kwa bingwa wa mashindano ya mwaka 2019 ikiwa ni ongezeko la asilimia 40.

Mshindi wa pili atapewa Dola 4 milioni ikiwa ni zaidi ya Dola 1.5 milioni iliyopewa Misri kwa kumaliza mshindi wa pili wa mashindano haya mwaka 2021.

Ongezeko pia litawafikia walioshia nusu na robo fainali ambao watapata zaidi ukilinganisha na ilivyokuwa hapo awali.

Timu iliyopoteza nusu fainali ilikuwa inapata Dola 2.2 milioni na ile ya robo fainali dola 1.18 milioni, mwaka huu timu itakayoishia nusu itapata Dola 2.5 milioni na robo fainali Dola 1.3 milionoi.

KWENGINE VIPI?

Mwaka huu kuna mashindano manne makubwa yatakayohusisha timu za taifa za mabara mbalimbali, ukiiondoa AFCON, kuna AFC Asian Cup 2023 (ASIA), Euro 2024 (Ulaya) na Copa America 2024 (Amerika Kusini).

Kwenye mashindano haya AFCON inashika nafasi ya tatu kwa kutoa pesa nyingi, ikiivuka Asian Cup.

Mshindi wa kwanza wa AFC Asian Cup 2023 anapata Dola 5 milioni tu, wakati wa pili ni Dola 3 milioni.

Mashindano ghali kwa upande wa timu za taifa kwa mwaka huu yatakuwa ni UEFA ambayo bingwa anapata Dola 30.9 milioni, hii ikiwa itashinda mechi zao zote za makundi, timu inayoshika nafasi ya pili itapata Dola 27.9 milioni.

Kwa upande wa Copa Amerika bingwa anapata anapata Dola 10 milioni na mshindi wa pili anapata Dola 5 milioni.

TIMU ZATANGAZA BONASI

Matajiri kutoka Afrika Kusini ambao chama chao cha mpira wa miguu kinaongozwa na Danny Jordaan, ambako pia anatoka mwenye jambo lake rais wa CAF, Patrice Motsepe, wenyewe wameahidi wachezaji wao wote ikiwa watafanikiwa kuchukua ubingwa kila mchezaji atapewa Euro 23,388 zaidi ya milioni 50 za Kitanzania.

Wachezaji wa timu ya taifa ya Nigeria, ‘Super Eagles’ wameahidiwa kwamba kila wakishinda mechi moja kwenye hatua ya makundi watapewa Dola 5,000.

Gambia inadaiwa kuandaa kiasi cha Dola 500,000 ambazo zitatumika kuwapa bonasi wachezaji wao kwenye kipindi chote cha mashindano, tayari imeshawapa Dola 5,000 kila mchezaji kwa kuwasili kwenye kambi ya timu ya taifa kuelekea mashindano haya.

SOMA NA HII  TROY DEENEY MALI YA BIRMIGHAM