Home Habari za michezo MOLOKO BADO YUPO AISEEE…..ISHU YAKE MPYA HII HAPA….

MOLOKO BADO YUPO AISEEE…..ISHU YAKE MPYA HII HAPA….

Habari za Yanga leo

Saa chache baada ya Yanga kutangaza kumtema winga Jesus Moloko Geita Gold iko naye mezani kwa mazungumzo ya kumsajili kwa mwaka mmoja.

Geita inamtaka Moloko kwenda kuongeza nguvu kwenye kikosi chao ikiutazama uzoefu wake na nidhamu kubwa aliyoonyesha akiwa Yanga.

Geita inapambana na Rayon Sport ya Rwanda kuwania saini ya winga huyo wa zamani wa AS Vita na Union Maniema zote za DR Congo.

Moloko ametemwa na Yanga kupisha usajili wa winga Mghana Augustine Okrah aliyetua klabuni hapo akitokea Bechem United ya nchini kwao.

Kwasasa Geita inapambana na Moloko juu ya mshahara wake na maslahi mengine binafsi wakati mazungumzo hayo yakiendelea.

Moloko bado anatamani kubaki zaidi Tanzania endapo atapata ofa nzuri itakayomshawishi kukubali mkataba.

SOMA NA HII  SAA KADHAA KABLA YA SIKU YA WANANCHI...EDO KUMWEMBE AIBUKA NA HILI KUHUSU WASHAMBULIAJI YANGA...AONYA..