Habari ya Simba leo
Habari za michezo

MFUMO BONASI ZA WACHEZAJI SIMBA WAPANGULIWA….MASTAA AKULIPWA MIL 100 KWA MECHI 5..

admin February 7, 2024 6:52 pm

Inaelezwa uongozi wa Simba SC, umeongeza hamasa ya kutafuta ushindi, ambapo kila baada ya ushindi kwenye michezo mitano wachezaji wanapewa Bonus ya shilingi milioni mia moja (Mil.100), ila kwenye michezo mitano ikatokea timu imepata matokeo ya sare au imepoteza basi inaanza upya mpaka pale watakapopata ushindi mfululizo kwenye michezo mitano.

Bonus hii haiondowi Bonus zao zilizopo kwenye mikataba yao kama timu ikishinda au timu ikibeba ubingwa, ambayo wamekubaliana awali kwenye kandarasi zao.

Kwa hiyo Simba SC, ikishinda michezo mitano mfululizo wachezaji pamoja na benchi la ufundi wanapata Bonus mara mbili.

Hii inakuja kama njia mbadala ya kupandisha morali za wachezaji ili waweze kuipambania timu kwenye upande wa mashindano ya ndani, haswa mara baada ya kupoteza ubingwa wa Ligi mara Mbili mfululizo.

Chanzo cha uhakika kutoka ndani ya Simba, kimetueleza kuwa wachezaji wamepokea kwa furaha mfumo huo mpya wa bonasi na kwamba ulianza kufanya kazi kwenye mechi dhidi ya Mashujaa.

Hata hivyo, mkakati huu unatajwa pia ni sehemu ya mapendekezo ya kocha mkuu Benchikha kwenye kuikifanya kikosi cha wekundu hao wa msimbazi kurudisha utawala wake wa soka la ndani.

AMERICAN ROULETTE MCHEZO RAHISI WA KUBASHIRI GURUDUMU LA NAMBA KWENYE MERIDIANBET.. HIVI NDIVYO WYDAD WALIVYOITUBULIA SIMBA KWA MASHINE HII YA MAGOLI….

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply