Habari za Yanga
Habari za michezo

ALLY KAMWE:- SIMBA vs AZAM SITAKI MTU AFUNGWE…ILA IKIBIDI BASI AHAMED ALLY ATALIA…

admin February 9, 2024 6:51 pm

Ofisa Habari wa Klabu ya Yanga, Ally Kamwe amesema kuwa anaomba dua mchezo wa leo kati ya Simba SC dhidi ya Azam FC umalizike kwa sare ili timu yao ishushe presha pale kwenye kilele cha msimamo wa Ligi hiyo.

Kamwe amesema hayo kuelekea mchezo huo utakaopigwa leo Ijumaa, Februari 9, 2024 katika Dimba la CCM Kirumba jijini Mwanza.

“Kiukweli mechi ya Simba SC dhidi ya Azam Fc, mimi sina timu nitakayoishabikia, matokeo ninayoyataka pale ni sare, ikitokea Mungu ameamua mmoja afungwe, basi afungwe makolo.

“Mimi sitaki yeyote afungwe kabisa, lakini kama ni lazima mmoja afungwe, basi dua yangu nipate mtu wa kumcheka. Azam yupo Ibwe na Zaka, dua yangu ya kuwacheka imeshaisha, basi afungwe Kolo, nimcheke Ahmed Ally na wenzake, wako wengi,” amesema Kamwe.

Yanga wapo nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa Ligi hiyo wakiwa na alama 37, michezo 14, Azam FC nafasi ya pili, alama 31, michezo 13 na Simba nafasi ya tatu, alama 29 na michezo 12.

MSUVA ABEBESHWA ‘ZIGO LA MISUMARI’ KWA WAARABU….DK ZAKE 90 ZA KWANZA ZAWA ‘KAVU’… BAADA YA KUONA KIWANGO CHA GUEDE…GAMONDI KAGUNA WEE..KISHA AKASEMA HAYA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply