Habari za Yanga SC
Habari za michezo

GAMONDI:- HAO TZ PRISONS HATUNA JINSI NAO….WACHEZAJI YANGA NI WACHOVU SANA…

admin February 10, 2024 12:19 pm

Kocha Mkuu wa Klabu ya Yanga, Miguel Gamondi amesema kuwa, amesema kuwa uchovu wa wachezaji na ubovu wa Uwanja wa Sokoine Mbeya unaweza kuufanya mchezo wao dhidi ya Tanzania Prisons ukawa mgumu.

Gamondi amesema hayo wakati akizungumza na wanahabari baada ya kumalizika kwa mchezo dhidi ya Mashujaa FC huku Yanga ikionekana kusua sua kupata matokeo katika michezo yake mitatu iliyocheza ikitoa sare moja na kushinda miwili, ikifunga mabao matatu na kufungwa bao 1.

Katika mchezo huo wa Ligi Kuu ya NBC, uliopigwa katika Dimba la Azam Complex, Chamazi, Yanga iliibuka na ushindi wa bao 2-1, dakika za lala salama.

“Tunajua mechi dhidi ya Tanzania Prisons itakuwa ngumu. Tunafahamu uwanja sio rafiki, wachezaji wana uchovu kutokana na mechi mfululizo lakini tutapambana.

“Ratiba yetu tutaondoka kesho mapema, tutafanya recovering, jambo la mhimu ni kwenda kupambana, ku-enjoy soka na kupata alama tatu, hao Tanzania Prisons nitaanza kuwafikiria kesho,” amesema Kocha Gamondi.

A-Z JINSI ‘MAZINGAOMBWE’ YA MUDATHIR YAHYA YANAVYOIBEBAGA YANGA CHAMAZI… KUHUSU TIMU KUSUA SUA….DICK JOB AVUNJA UKIMYA YANGA…AFUNGUKA KINACHOWAKWAMISHA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply