Habari za Simba leo
Habari za michezo

KISA SARE NA AZAM JANA ….MABOSI SIMBA WAIBUKA NA TAMKO HILI….”MATOKEI SI MAZURI….”

admin February 10, 2024 12:34 pm

BAADA ya kuambulia sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Azam FC, mabosi wa Simba wamekuja na mpango kazi kwa ajili ya mechi znazofuata.

Ipo wazi kuwa Februari 9 ubao wa Uwanja wa CCM Kirumba ulisoma Simba 1-1 Azam FC.

Prince Dube alipachika bao dakika ya 14 huku Clatous Chama akifunga bao la kuweka usawa dakika ya 90.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amesema:”Tunamshukuru Mungu kwa matokeo tuliyopata, Si mazuri sana na si mabaya sana.

“Tunawapongeza wachezaji wetu kwa kupambana na kuvuna alama moja kwani bila upambanaji wao tusingeipata,

“Hili limekwisha, Sasa tunaangalia zaidi mechi ijayo.

Asanteni Mwanza, Asante kanda ya Ziwa, Asanteni wana Simba. Jicho letu sasa ni Feb 12 dhidi ya Geita Gold hapa hapa Kirumba,”.

Simba ipo nafasi ya tatu kwenye msimamo na pointi 30 Azam FC nafasi ya pili na pointi 32.

HII HAPA SLOT YA USHINDI KWENYE MERIDIANBET CASINO…SHINDA MPAKA MARA 15 YA DAU LAKO.. HAWA HAPA WALIOIFANYA SIMBA KUTAMBA AFRICA NZIMA KIBABE….AL AHLY WANAJUA UKWELI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

One response to “KISA SARE NA AZAM JANA ….MABOSI SIMBA WAIBUKA NA TAMKO HILI….”MATOKEI SI MAZURI….””

  1. Yunus said mbonde says:

    Japo tumepata sare tusife moyo maisha yaendelee

Leave a Reply