Home Habari za michezo AZIZ KI ALIVYOITESA YANGA KWA DAKIKA 356….ISHU NZIMA IKO HIVI…

AZIZ KI ALIVYOITESA YANGA KWA DAKIKA 356….ISHU NZIMA IKO HIVI…

Habari za Yanga

Kiungo mshambuliaji wa Yanga Stephanie Aziz Ki amerejea kazini na mchezo wa ligi uliopita akipewa dakika 4 za mwisho lakini takwimu zikathibitisha jinsi ambavyo kikosi hicho kilikosa huduma yake.

Aziz KI amezikosa dakika 356 za ligi tangu iliporejea ikiwa ni mechi tatu dhidi ya Mashujaa na Dodoma Jiji timu yake ikiwa nyumbani na pia akakosa mechi ya Kagera na ile ya Prisons ambayo aliingia dakika ya 86, na kuifanya timu yake licha ya kushinda ikionekana kupata shida ya kuzalisha mabao ya kutosha.

Takwimu zinaonyesha kuwa Aziz Ki ameifungia Yanga mabao 19 kwa maana ya mabao 9 ya msimu uliopita na 10 ya mpaka sasa msimu huu, amefunga mabao 11 nje ya eneo la hatari ambapo katika hayo 7 aliyafunga msimu uliopita wakati 4 akiyafunga msimu huu.

Ndani ya mabao hayo 11, ni mabao matano ameyafunga kwa mpira wa adhabu ndogo huku sita yakitokana na maamuzi yake ya kujaribu mashuti kwa mbali.

Tangu ligi irejee kupisha Fainali za Mataifa Afrika (Afcon 2023), Yanga imecheza mechi 4 ikifunga mabao matano lakini hakuna hata bao moja lililofungwa nje ya eneo la hatari, huku yote yakifungwa kama siyo ndani ya sita basi nje kidogo ya eneo hilo.

Takwimu zinaonyesha kuwa Aziz Ki amefunga mabao 5 ya eneo la hatari kwa misimu yote miwili, ameyafunga msimu huu wakati msimu uliopita hakuwa na bao alilolifunga ndani ya eneo la hatari.

Aidha kiungo huyo mshambuliaji ana mabao matatu ya penalti aliyoyafunga kwa misimu miwili akiweka wavuni penalti 2 msimu uliopita wakati msimu huu akiwa nayo moja.

Katika michezo iliyopita, Yanga ilionekana kushindwa kufanya vizuri kwenye mipira mingi ya adhabu na haikuwa na mpigaji maalum wa mipira hiyo, lakini wakati mwingine ilishindwa kupata mabao mengi kutokana na wachezaji wote kusubiri kuingia kwenye eneo la hatari badala ya kujaribu kutoka mbali kama ambavyo kiungo huyo amekuwa akifanya.

SOMA NA HII  YANGA YAPIGA HESABU YA KUTWAA MAKOMBE