WAKIWA ugenini kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara wameshuhudia ubao wa Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo ukisoma JKT Tanzania 0-1 Simba ukiwa ni mzunguko wa kwanza.
Simba inakomba pointi tatu na kufikisha pointi 36 kibindoni baada ya kucheza mechi 15 sawa na watani zao wa jadi Yanga kwenye upande wa mechi ndani ya ligi.
Nafasi ya pili wanabaki kwa bao la kiungo Clatous Chama dakika ya 33 ambaye alipachika bao hilo kwa utulivu mkubwa ikiwa ni baada ya Simba kukosa nafasi tatu za wazi kufunga kwenye kipindi cha kwanza.
JKT Tanzania ni Sixtus Sabilo huyu alikuwa na zali la kutaka kufunga ambapo alikutwa kwenye mtego wa kuotea mara moja kipindi cha kwanza na alipiga mashuti yaliyolenga lango mara tatu kipindi cha kwanza.
Kipindi cha pili Matheo Athony alikuwa kwenye nafasi nzuri ya kufunga bao kwa Ayoub Lakred bahati haikuwa kwake shuti lake lilikwenda nje kidogo ya lango na kuwa shot on target.
Mwendelezo wa Simba kutengeneza nafasi nyingi na kushindwa kuzitumia huku kipindi cha pili wakitumia muda mwingi kujilinda na kushambulia kwa kushtukiza.
Mzunguko wa kwanza wa Ligi umemalizika Simba ikiwa nafasi ya pili tukiwa na alama 36 baada ya kucheza mechi 15.