Home Habari za michezo HUU HAPA UKWELI KUHUSU NOVATUS DISMAS ‘KUPIGWA CHINI’ SHAKHTAR DONETSK….

HUU HAPA UKWELI KUHUSU NOVATUS DISMAS ‘KUPIGWA CHINI’ SHAKHTAR DONETSK….

Habari za Michezo

Maswali yalikuwa mengi ni kwa nini Novatus Dismas hapewi nafasi ya kucheza Shakhtar Donetsk? Ila pia wengi wakashangazwa kwa nini mchezaji wa kikosi cha kwanza moja kwa moja akawa anakaa jukwaani na sio kwenye benchi?

Mchambuzi wa masuala ya soka na msimamizi wa wachezaji Bongo, Shaffih Dauda amesema kuwa tatizo kubwa lilikuwa ni mambo ya biashara lakini kwa sasa wameshazungumza na kuyamaliza.

“Novatus Dismas alisajiliwa kwa mkopo pale Shakhtar Donetsk na bahati mbaya kocha aliyemsajili alifukuzwa na kocha huyu alimsajili kwa sababu waliwahi kufanya kazi pamoja nyuma nchini Israel

“Na bahati mbaya zaidi sera ya Shakhtar Donetsk ni kufanya biashara ya kuuza vijana kwa hiyo ikawa ni ngumu kwao kumpa nafasi mchezaji ambae sio mali yao wakihofia kama watampa nafasi ya kuonekana uwezo wake na kuwa sokoni watakuwa wameitangaza biashara ya timu nyingine.

“Ila kwa sasa nimeona kocha wa sasa ameamua kumpa nafasi na kwenye michezo mitatu ya nyuma ya Kirafiki alimpa nya kucheza hii ni ishara kuwa kocha ameshajua uwezo wake hasa baada ya kumpa nafasi kwenye mchezo wa hisani ambao walicheza nchini Japan wakati wa mapunziko.

“Binafsi naona kama watakuwa wameshafanya makubaliano nyuma ya pazia kati ya Shakhtar Donetsk na Zulte Weregem kwenye kipengele cha ule mkataba wa awali ambapo kulikuwa na kipengele cha kumnunua moja kwa moja, kwa hivyo naona kama mwishoni mwa msimu huu Novatus Dismas atakuwa mchezaji wa moja kwa moja ndani ya Shakhtar Donetsk.

“Hata baada ya mashindano ya AFCON Tanzania kutolewa Shakhtar Donetsk walituma Email kuwa wanamuhitaji haraka kambini pale nchini Uturuki hata Visa yake iliombewa nchini Ivory Coast, nimeongea nae Novatus ameniambia kwa sasa anayaona matumaini mbele yake,” amesema Shaffih Dauda.

SOMA NA HII  BAADA YA KUONA KIWANGO CHA SAKHO SIKU ZA HIVI KARIBUNI...PABLO AKUNA KICHWA WEE...KISHA ANENA HAYA..