Uwanja mpya Arusha
Habari za michezo

HII HAPA TAREHE YA KUANZA KUJENGWA UWANJA MPYA WA ARUSHA…MAMBO NI πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯…

admin February 18, 2024 8:08 pm

Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo, Ally Mayay amesema waandaaji wa fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon) 2027; Tanzania, Kenya na Uganda kila nchi itapaswa kuwa na viwanja vitatu na kwamba Tanzania tayari inavyo viwili Benjamin Mkapa na Amaan Zanzibar hivyo umebaki uwanja mmoja ambao utajengwa Arusha.

Mayay amesema mambo ya tathimini yalishakamilika na sasa wako katika hatua ya mapatano, na kwamba ujenzi wa uwanja huo mpya wenye uwezo wa kubeba watu 30,000 utaanza kujengwa mwezi ujao.

β€œTuko kwenye hatua za mwisho na mkandarasi wa ujenzi wa uwanja wa Arusha, mpaka Desemba 2025 CAF watakuja kuangalia tayari utakuwa umekamilika.”

NYASI BANDIA AMAAN

Mayay amesema nyasi bandia za Uwanja wa Amaan zitaondolewa na kupandwa nyasi asilia ili ukidhi vigezo vya michuano hiyo ya kimataifa.

β€œUwanja wa Amaan ushakamilika kwa asilimia 100. Kilichobaki ni kubadili tu zile nyasi bandia na kupanda nyasi asilia, jambo ambalo linachukua muda mfupi tu wa kuanzia sita,” amesema na kuongeza: β€œWatu wengi wanazungumzia kuhusu viwanja vya mechi tu. Timu zitakuwa na viwanja vya wazi kwa ajili ya mazoezi ambavyo zinaweza kufanya mazoezi muda wowote, timu inakabidhiwa uwanja wake wa mazoezi na inaweza kufanya mazoezi muda wowote itakaotaka iwe mchana au usiku.

β€œKwa Zanzibar vipo na vinaendelea kuandaliwa. Arusha maeneo ya wazi yapo. Kwa Dar es Salaam kuna Gymkhana, JK Park na hata Leaders Club patatengenezwa kukidhi viwango vinavyohitajika ikiwa ni pamoja na kuwekewa taa.”

Mayay amesema hayo leo Februari 14, 2024 wakati akichangia mjadala wa Mwananchi Space ulioandaliwa na Mwananchi Communications Ltd, wenye mada isemayo “Tanzania imejifunza nini kupitia AFCON 2023, ikijiandaa 2027?”

TAIFA STARS KUSHIRIKI MASHINDANO MAPYA YA FIFA….MCHONGO KAMILI UKO HIVI… KUELEKEA MECHI YA CAF…SIMBA WAISHTUKIA JAMBO HILI IVORY COST….

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply