Habari za Simba SC
Habari za michezo

HII HAPA SABABU KUBWA YA JOHN BOCCO KUPIGWA ‘PANGA’ SAFARI ZA IVORY COAST….

admin February 22, 2024 2:44 pm

Meneja wa timu ya Simba SC, Mikael Igendia amesema nahodha wa timu John Bocco hakuwa sehemu ya msafara kwa sababu ya majeraha.

Igendia amefunguka hayo akiwa nchini Ivory Coast ambako timu imewasiri kuwakabili ASEC Mimos kesho kutwa Ijumaa Februari 23.

“Wachezaji watatu muhimu ambao hatujasafiri nao ni Ayoub Lakred, Willy Onana na John Bocco ambaye alipata majeraha tulipokuwa tunashiriki Kombe la Mapinduzi,” alisema Igendia.

Meneja huyo alisema Bocco atakapopona majeraha yake, atajiunga na timu na wenzake.

Simba kesho watashuka dimbani kupepetana na wenyeji wao Asec Mimosas katika mchezo wa hatua ya makundi ligi ya Mabingwa Afrika.

Ni ushindi pekee ambao Simba wanauhitaji katika mechi ya kesho haswa ukizingatia wako kwenye kundi gumu huku wakizidiwa alama na Asec wanaoongoza kundi hilo.

Endapo Simba watapata ushindi kesho utawaweka kwenye wakati mzuri zaidi wa kufuzu kwenda hatua ya robo fainali.

Kwenye kundi lao, mpaka sasa ni Asec Mimosas ambao wameshajihakikishia kwenda hatua ya robo fainal mpaka sasa.

MANARA :- TFF IMFUKUZE KAZI AMROUCHE….ANAIHUJUMU YANGA MCHANA KWEUPEEE… MAGOLI YA GUEDE YAMEFICHWA NA HUYU….MKITAKA ATUPIE SANA AWEKWE SAWA KWANZA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply