Home Habari za michezo MAGOLI YA GUEDE YAMEFICHWA NA HUYU….MKITAKA ATUPIE SANA AWEKWE SAWA KWANZA…

MAGOLI YA GUEDE YAMEFICHWA NA HUYU….MKITAKA ATUPIE SANA AWEKWE SAWA KWANZA…

Habari za Yanga leo

Mchambuzi wa masuala ya soka nchini upitia Clouds Media, Master Tindwa amesema kuwa mabao ya mshambuliaji mpya wa Yanga, Joseph guede yapo wenye miguu ya kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Augustine Okrah raia wa Ghana.

Kauli hiyo ya Tindwa inakuja ikiwa ni saa chache baada ya guede aliyekuwa akisubiriwa na Wananchi kwa muda mrefu kufunga bao la kwanza tangu asajiliwe na Yanga kwenye dirisha dogo msimu huu na kutoa gundu ya kukosa kosa mabao anapopata nafasi.

Guede alifunga mabao mawili katika mabao 5-0 walioshinda Yanga jana dhidi ya Polisi Tanzania huku akikosa mabao mengine mawili ya wazi huku mabao yote aliyofunga akipewa assists na Okrah ambaye pia amesajiliwa kwenye dirisha dogo.

“Magoli yote ya Guede yametoka mguuni kwa Okrah licha ya kuwa kuna nafasi moja amepoteza, tunasema kwamba magoli ya Guede yapo mguuni kwa Okrah”

“Leo hii sio Guede peke yake ambaye amefungua account ya magoli, Okrah pia ameanza vizuri,” amesema Master Tindwa.

SOMA NA HII  HAYA SASA...KUHUSU DILI LAKE NA YANGA...LILOPO MEZANI...AFUNGUKA YOTEE...MGUNDA ASEMA UKWELI...