Habari za Simba SC
Habari za michezo

KISA SARE YA JANA…BENCHIKHA ‘KINYOONGEEEE’ KASEMA HILI KWA MASTAA WA SIMBA…

admin February 24, 2024 1:46 pm

Kocha Mkuu wa Yanga Abdelhak Benchikha amewapongeza wachezaji kwa kucheza soka safi licha ya kupata sare ugenini dhidi ya ASEC Mimosas katika mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Benchikha amesema ameridhishwa na jinsi timu ilivyocheza kwa umoja na kushirikiana na kusababisha kupatikana kwa pointi moja muhimu ugenini.

Benchikha ameongeza kuwa kwa sasa hakuna muda wa kupumzika maandalizi ya mchezo wao wa mwisho wa hatua ya makundi dhidi ya Jwaneng Galaxy ambao utapigwa mwishoni wa juma lijalo yanaanza.

“Tunaushukuru Mungu kwa kutuwezesha kupata pointi moja ugenini, kama nilivyosema awali isingekuwa mechi rahisi lakini tumepambana hadi mwisho.

“Nawapongeza wachezaji wangu kwa kazi kubwa waliyofanya sasa tunarejea nyumbani kwenda kujiandaa na mchezo wa mwisho dhidi ya Jwaneng,” amesema Benchikha.

BAADA YA KUBANWA IVORY COAST JANA….SIMBA KUJA KIVINGINE ‘GAME’ NA JWANENG… HUYU HAPA NYOTA WA YANGA ALIYELAMBA SHAVU LA UBOSI KWENYE ‘TFF’ YA GHANA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply