Habari za Yanga SC
Habari za michezo

JINSI GUU LA PACOME LILIVYOZUA BALAA KWA CR BELZOUIDAD….MAKOCHA WOTE KICHWA CHINI…

admin February 26, 2024 11:49 am

Baada ya bao la tatu la Kenedy Musonda nilimuona kocha wa Belzouidad akiwa ameshika kiuno hajui cha kufanya. Wakati huo wasaidizi wake wote walikuwa wameketi kinyonge katika benchi hawajui cha kufanya!

Lugha iliyokuwa inazungumzwa na Macho yao ni kwamba “Tunaona magumu wanayopitia wachezaji wetu lakini hatujui cha kufanya”. Walikuwa wamenyoosha mikono juu kile walichokuwa wanafanyiwa na Yanga.

Ni ngumu sana kumtaja mchezo mmoja wa Yanga ambaye anastahili kuwa mchezaji bora wa mchezo. Kuanzia kwa Djigui Diarra mpaka kule juu kabisa kwa Kenedy Musonda, kila mmoja alikuja na viatu vyake vya mchezo

Kuna yule fundi wa Afrika, yule Zizzou wa Algeria aliyeikataa Algeria halafu kuna Zizzou wa Ivory Coast. Zizou wa Yanga Afrika. Yule mwamba Pacome Zouzoua anajua mpira kuliko wanaojua. Pacome is a baller.

Aziz Ki ni ufunguo wa kufungua vitasa katika milango migumu. Kuhusu Mudathir?? Ile ni sindano ndogo inayoshona makoti makubwa. Na Ibra Bacca naye aandikwe..

Ile ndio Yanga Afrikaa katika kilele cha ubora wake. Robo fainali kibabe sana

GAMONDI:- KUNA WATU WALITUCHEKA KABLA YA MECHI…BAADA YA MECHI WAKAONA AIBU WAO… WAKATI YANGA WAKIFURAHIA NA CAF….VITA NI MBICHI KWA FEI TOTO NA AZIZ KI….ISHU YAO IKO HIVI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply