FT:- SIMBA 6-0 TRA
Habari za michezo

FT:- SIMBA 6-0 TRA…..KANOUTE KAMA PACOME TU…..BENCHIKHA AWATISHA JWANENGA KIBABE….

admin February 28, 2024 10:13 pm

TIMU ya Simba imetinga kibabe hatua ya 16 bora ya michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) baada ya kuibuka na ushindi mnono wa mabao 6-0, dhidi ya TRA ya Kilimanjaro katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex ,Chamanzi.

Katika mchezo huo wa hatua ya 32 bora, shujaa wa Simba ni kiungo wa kikosi hicho, Sadio Kanoute aliyefunga mabao matatu ‘hat-trick’ huku mengine yakifungwa na Ladaki Chasambi, Pa Omar Jobe na Freddy Michael waliofunga moja kila mmoja wao.

Ushindi huo kwa Simba ni salamu tosha kwa wapinzani wao Jwaneng Galaxy watakaokutana nao Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam katika hatua ya makundi kuwania tiketi ya kufuzu robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Simba iliyokuwa kundi ‘B’ la michuano hiyo inahitaji ushindi kwenye mchezo huo ili kukata tiketi ya kufuzu hatua ya robo fainali kwani itafikisha pointi tisa na kushika nafasi ya pili nyuma ya vinara ASEC Mimosas iliyofuzu na pointi 11.

Kikosi hicho chenye pointi sita sawa na Wydad Casablanca ya Morocco, endapo kitashinda mchezo huo kitafuzu moja kwa moja bila ya kujali matokeo ya mchezo mwingine wa kundi hilo utakaopigwa kati ya Wydad itakayoikaribisha ASEC Mimosas.

Licha ya Simba kuhitaji ushindi ila ina kumbukumbu mbaya ya mwaka 2021 ilipoondoshwa na Jwaneng kwenye duru la kwanza Ligi ya Mabingwa kwa bao la ugenini baada ya mechi ya kwan za kushinda 2-0, kisha marudiano kuchapwa 3-1, Benjamin Mkapa.

Hadi sasa tayari timu sita zimeshafuzu robo fainali ambazo ni ASEC Mimosas (Ivory Coast), Yanga (Tanzania), Mamelodi Sundowns (Afrika Kusini), Al Ahly (Misri), Petro de Luanda (Angola) na TP Mazembe kutoka nchi ya Kidemokrasia ya Congo.

WAKATI MASHABIKI YANGA WAKIENDELEA KUMUIMBA….AKILI YA PACOME INAWAZA HILI TU KWA SASA.. PACOME:- MECHI NA AL AHLY DUA ZENU ZINAHITAJIKA SANA….NI WAGUMU MNOO..

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply