TAARIFA kutoka nchini Misri zinadai kuwa, straika wa kikosi cha Pyramid Fiston Mayele ameandika barua ya kuomba kuvunja mkataba na timu yake hiyo huku Simba wakitajwa kutaka kumsajili kwenye dirisha lijalo la usajili.
Mayele amefikia uamuzi huo mgumu baada ya kushindwa kupata namba ya kudumu kama alivyotarajia ikidaiwa kwamba, anataka kurejea Ligi Kuu Tanzania Bara huku chaguo lake la kwanza likitajwa kuwa ni Simba.
Ikumbukwe kwamba hivi karibuni kulikuwa na taarifa ya mshambuliaji huyo kutaka kutolewa kwa mkopo na kuhusishwa timu mbili hapa nchini ikiwemo Simba na Azam FC.
Mtoa habari kutoka nchini humo, amesema baada ya kutopata nafasi nyota huyo ameamua kutaka kuandika barua ya kuvunja mkataba wake kwa lengo la kuakiangalia changamoto sehemu nyingine ambapo atapata nafasi.
Kwa hali ilivyo Mayele anatajwa kutua ndani ya kikosi cha Simba kipindi cha dirisha kubwa kuongeza nguvu na kuimarisha katika safu hiyo ya ushambuliaji.
“Awali klabu ya mchezaji huyo ilipanga kumtoa kwa mkopo kwa moja ya klabu ambayo ilikuwa ikimuhitaji Simba na Azam FC wakihusishwa lakini Wekundu wa Msimbazi walipewa kipaumbele kikubwa kwa sababu ya kuhitaji mshambuliaji.
Sasa nyota huyo anataka kuvunja mkataba na klabu yake hiyo ni suala la Simba kuchangamkia fursa kuweza kunasa saini yake mapema,” amesema mtoa habari huyo.
Kulingana na Changamoto ya safu ya ushambuliaji ya Simba hivi karibuni, kipindi cha dirisha dogo timu hiyo iliamua kuwasajili Pa Omar Jobe na Freddy Michael ambao wamechukuwa nafasi ya Jean Baleke na Mosses Phiri.
Hali hiyo bado haijaweza kutulia kwenye safu hiyo na Simba wanatazamiwa kuwakwenye mpango wa kutaka kuanza mazungumzo na Mayele ili kurejea nchini kwa mara nyingine akiwa na jezi nyekundi na nyeupe .
Mayele aliyesajiliwa na Pyramid FC akitokea Yanga baada ya kumuuza huku nafasi yake ikichukuliwa na Hafiz Konkoni ambaye naye hakuweza kuushawishi uongozi na kuondolewa na sasa wamemleta Joseph Guede kurithi mikoba ya raia huyo wa DR Congo.
Heri Mayele audi Yanga vinginevyo mambo yake inawezekana yakawa sio anavyotarajia.
Aje tu simba hatuna striker, hivyo akija tutakuwa tumetoka mahali fulani
Comment: mayele heri aje simba mana hatuna mshambuliaj aliye bora
Comment:mayele akitua simba kiwango chake kitazidi kuongezeka mana kuna mafundi wengi simba