Home Habari za michezo WAKATI GUEDE AKIENDELEA KUJITAFUTA YANGA….FREDY APATA WA KUMTETEA SIMBA SC…

WAKATI GUEDE AKIENDELEA KUJITAFUTA YANGA….FREDY APATA WA KUMTETEA SIMBA SC…

Habari za Simba leo

Kocha wa makipa wa Simba Daniel Cadena, amesema benchi la ufundi la timu hiyo linaamini kuwa mshambuliaji wao mpya, Fredy Michael, ataanza kufunga mabao hivi karibuni pamoja na kwamba anakosa sana nafasi za wazi.

Mshambuliaji huyo raia wa Cameroon alisajiliwa na Simba dirisha dogo akitokea Green Eagles ya Zambia na tayari amecheza mechi nne za timu hiyo dhidi ya Mashujaa, Tabora United, Azam na Geita Gold na kufunga bao moja.

Akizungumzia kiwango cha nyota huyo katika mechi hizo, Cadena alisema licha ya kuonekana kukosolewa pale anapokosa nafasi lakini benchi la ufundi linamuamini na litaendelea kumsaidia kuzoea mazingira kwani ni sehemu ya mipango ya kikosi hicho katika mechi zijazo.

“Anaweza kuwa bado hajazoea mazingira na kuelewana na wachezaji waenzake lakini sisi tunamuamini kabisa kwenye mipango yetu na kocha (Abdelhack Benchikha) na sisi wasaidizi wake tutaendelea kumpa nafasi na kumsaidia katika mechi zijazo,” alisema Cadena.

Aliongeza kwamba, mchezo uliopita dhidi ya Geita Gold, walipata ushindani mkubwa na walikabiliana na timu nzuri huku akilia na ratiba kuwa inawabana na mazingira ya Uwanja wa CCM Kirumba kuwasumbua.

“Tumeondoka na pointi tatu lakini ilikuwa mechi ngumu kwetu kucheza katika uwanja huu na tulikuwa na ratiba ambayo tunapaswa kucheza mechi tano ndani ya siku 12, jambo ambalo ni gumu katika siku mbili tu maandalizi huwezi kufanya mazoezi ya kutosha na kurejesha miili vizuri, kwa hiyo ilikuwa ngumu kupata hizo pointi tatu tulizozipata leo kwahiyo tunapaswa kuendelea kupambana kila siku na kufanya vizuri.

“Sasa tumemaliza hivyo tunakwenda kwenye plan tena ya michezo mingine minne kuhakikisha kwamba tunapata alama nyingi kama ilivyo malengo yetu kwamba msimu huu na sisi tunakuwa mabingwa,” alisema.

SOMA NA HII  BAADA YA KUSHINDA MECHI YAKE YA KWANZA KAMA KOCHA MKUU SIMBA....MATOLA FUNGUKA ALICHOKIFANYA NYUMA YA PAZIA...