Habari za Yanga leo
Habari za michezo

KUHUSU KUFUNGA SANA MAGOLI …..MUDATHIR HUYU HAPA….AANIKA KILICHONYUMA YAKE…

admin March 1, 2024 10:27 am

Kiungo wa Klabu ya Yanga, Mudathir Yahya, amekuwa na wakati mzuri sana msimu huu ndani ya kikosi cha Young Africans SC kutokana na aina ya uchezaji wake.

Staili yake ya uchezaji huku akiwa anatumika kwenye nafasi tofauti uwanjani, ndiyo imemfanya kuwa bora zaidi hadi sasa na kuweka rekodi mpya.

Kiungo huyo juzi Jumamosi alianza kufunga goli la kwanza katika ushindi wa magoli 4-0 dhidi ya CR Belouizdad ukiwa ni mchezo wa Kundi D wa Ligi ya Mabingwa Afrika uliochezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Kuhusu ubora wake huo, Mudathir amesema: “Huu ndiyo msimu wangu bora katika maisha yangu ya soka, kwanza nimeweza kucheza nafasi tofauti ambazo naambiwa ninazitendea haki.

“Pili msimu huu mpaka sasa nimeweza kufunga magoli 8, mawili Klabu Bingwa na 6 Ligi Kuu, ninaamini mengi mazuri yanakuja.

“Napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru Wananchi kwa kutuonesha mapenzi makubwa na kutochoka kutupa sapoti hata pale tunapokuwa nyuma kimatokeo wamekuwa na nguvu ya kutuhamasisha tupambane. Nawaahidi mengi mazuri.”

UANZE MWEZI MARCH KWA KUVUNA KIBUNDA CHA MERIDIANBET CASINO NA SLOT HII MPYA.. MHHH…HAPANA..KWA HAYA ANAYOANYIWA PACOME NA YANGA…MAYELE AELEZWE UKWELI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply