Home Habari za michezo HII HAPA SIKU YA SIMBA, YANGA KUJUA ‘VIBONDE’ WAO WA ROBO FAINAL...

HII HAPA SIKU YA SIMBA, YANGA KUJUA ‘VIBONDE’ WAO WA ROBO FAINAL CAF…

Habari za Michezo

Nchi hivi sasa inaendelea kurindima kutokana na magwiji wa soka nchini, kutoka mitaa ya Msimbazi na twiga (Jangwani), Simba na Yanga kutinga hatua ya robo fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kuna historia zimeandikwa hapa. Awali, timu mbili za Tanzania kuingia hatua ya makundi kwa mara ya kwanza katika michuano hiyo.

Pili, kuna historia ya klabu mbili nchini kuingia hatua ya robo fainali kwa mara ya kwanza katika michuano hiyo. Tatu, Tanzania ndiyo Taifa pekee limeingiza klabu mbili katika robo fainali ya CAF kwa msimu huu.

Ukiangalia kwa undani zipo historia sasa, zinazohusu klabu husika. Simba inatinga kwa mara nne hatua ya robo fainali katika michuano, huku Yanga ikitinga kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwake.

Haya yote ni matunda ya uwekezaji, uongozi bora na usajili mzuri wa wachezaji wenye ubora unaotakiwa na uzoefu. Kongole liende kwa vilabu vyote.

Ni wakati wa kutengeneza historia mpya katika soka la ushindani kwa ngazi ya Afrika kwa kusaka tiketi ya nusu fainali, walau kwa klabu moja, ikishindikana kupeleka zote. Dua za Watanzania zipo na nyinyi, mashujaa wetu!

Lakini dua za wapiga mikeka zipo kwenye mchakato wa droo ya hatua ya robo fainali, ambayo ndiyo inayosubiriwa kwa hamu kujua mpinzani wa kila mmoja wao. Droo ya CAF Champions League hatua ya robo fainali itafanyika tarehe 13/03/2024 jijini Cairo nchini Misri.

Wakati kulwa na doto wa Kariakoo wakisubiri droon kujua wapinzani wao, wazee wa mikeka watakuwa mubashara wakiangalia namna gani mikeka yao wanaichezesha kuhakikisha wanapiga mkwanja kupitia SportPesa.

Wazee wa mikeke wanaangalia kundi la timu vinara (Chungu A) dhidi ya wale walioshika nafasi za pili (Chungu B). Kwa hali ilivyo, Yanga anaweza kucheza dhidi ya Mamelodi Sundowns, Petro de Luanda au Asec Mimosas. Simba wao wanaweza kukutana na Mamelodi Sundowns, Al Ahly au Petro de Luanda.

SOMA NA HII  USIPANGE KUKOSA NAKALA YAKO YA GAZETI LA CHAMPIONI JUMATATU