Home Habari za michezo AHMED ALLY:- TUKIANZA KUSEMA MCHEZAJI HUYU HAFAI , YULE FAHAI TUTAZIDI KUPOTEANA…

AHMED ALLY:- TUKIANZA KUSEMA MCHEZAJI HUYU HAFAI , YULE FAHAI TUTAZIDI KUPOTEANA…

Habari za Simba

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally amewaomba mashabiki kuendelea kupa sapoti timu yao licha ya kupata matokeo mabaya kwenye mchezo wao wa jana.

Ahmed amesema hayo jana baada ya kumalizika kwa mchezo wa Ligi Kuu ya NBC huku SImba SC wakikubali kichapo cha bao 2-1 kutoka kwa Tanzania Prisons katika Uwanja wa CCM Jamhuri Morogoro.

“Kuumia pasi na shaka wameumia, kila Mwanasimba ameumia kutokana na matokeo haya. Watu wa Morogoro watakuwa wameumia sana kwa sababu walikuwa na shauku ya kuiona Simba ya moto na walikuwa na matarajio na matumaini makubwa kwamba leo (jana) ile Simba ya hatari inakwenda kuiona mubadhara kwa macho yangu kwa matokeo haya wamekuwa disappointed.

“Lakini niwambie tu kwamba ndiyo matokeo ya mpira wa miguu, kuna wakati tunapata matokeo ya kutuumiza kama haya. Tuwaombe radhi wana Morogoro kwa hiki ambacho kimetokea. Tuendelea kuwaomba sapoti yao, mchango wao na nguvu yao kuendelea kuisapoti Simba yao.

“Tayari tumeshapoteza alama tatu, hata tukisema huyu hafai, huyu kafanya hivi, huyu vile, bado haiwezi kufuta matokeo ambayo tumeyapata.

“Tumeyapokea matokeo haya na kuangalia wapi kumekuwa na madhaifu kwa siku ya leo (jana) na kwenda kuyafanyia kazi katika michezo inayokuja. Ya leo yamewaumiza, lakini tugange yajayo, tusiiache timu peke yake pasi na mashabiki,” amesema Ahmed.

SOMA NA HII  BAADA YA KUPITIA UKAME MWINGI...HATIMAYE TATIZO LA BOCCO LAPATA DAWA...CHAMA ATAJWA KUHUSIKA...