Habari za Michezo
Azam FC

DUBE AENDELEA KUWAPELEKEA MOTO AZAM FC….

admin March 7, 2024 12:54 pm

MAMBO yanazidi kupamba moto kwenye sakata la mshambuliaji, Prince Dube ambaye ameamua kufuta utambulisho wa timu ya Azam FC kwenye akaunti yake ya mitandao ya kijamii ‘Instagram’.

Ipo hivi; juzi uongozi wa Azam FC umekiri kupokea barua ya mchezaji huyo kwa ajili ya kuvunja mkataba na ukakubali kwa kumtaka kufuata utaratibu unavyotaka kulingana na makubaliano ya pande mbili.

Wakati hilo bado halijatolewa ufafanuzi juu ya yeye kuamua kufuata taratibu za mkataba ikiwamo kurejesha fedha zilizopo katika dili jipya zinazodaiwa kuwa Dola 300,000 (zaidi ya Sh700 milioni), mshambuliaji huyo ameondoa utambulisho kwamba ni mchezaji wa timu hiyo sambamba na kufuta picha zote alizovaa jezi ya Azam FC.

Dube ambaye anahusishwa kujiunga na Yanga, mbali na kuondoa utambulisho huo amefuta picha zote zenye jezi za timu hiyo na kuacha zile za maisha ya kawaida, sambamba na za timu alizopita miaka ya nyuma.

Sakata la Dube liliibuka baada ya mchezaji huyo kutoongozana na Azam FC kwenda kwenye mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Tanzania Prisons huku ikielezwa kuwa anasumbuliwa na majeraha.

Taarifa za uhakika niĀ  kuwa mchezaji huyo ana mgomo baridi kutokana na suala linalohusisha mkataba wake.

Na juzi Ofisa Habari wa klabu hiyo, Zaka Zacharia aliibuka na kutoa ufafanuzi akikiri kuwa uongozi umepokea barua ya mshambuliaji huyo kuomba kuvunjiwa mkataba.

ROBERTINHO:- PACOME ALINIFUKUZISHA KAZI SIMBA….KUHUSU UBORA WA CHAMA MHHH….. KUELEKEA MECHI IJAYO YA LIGI….ZAHERA AWAPIGA MKWARA WA KUFA ‘NTU’ YANGA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply