Home Habari za michezo SIMBA MNAMTAKA PACOME…..?., HII HAPA MASHINE YA KAZI ..AKITUA TU BONGO SHIDA...

SIMBA MNAMTAKA PACOME…..?., HII HAPA MASHINE YA KAZI ..AKITUA TU BONGO SHIDA ZOTE KWISHA…

Habari za Simba leo

Moja ya eneo ambalo Yanga wanawazidi Simba katika misimu hii miwili ya utawala wao basi ni eneo la usajili ambapo Yanga Rais wao Injinia Hersi Said yuko mstari wa mbele katika usajilu.

Nini ambacho nataka kusema katika hili,angalia usajili wa Zidane wa Afrika Pacome Zouzoua namna ambavyo Wananchi Yanga wananufaika nae kwa msimu huu.

Angalia kiwango cha Max Nzengeli aliyefunga goli mbili dabi ya Kariakoo. Andiko hili lengo lake ni kuwapa mchongo katika dirisha la kubwa la usajili kwamba kuna dhahabu pale Asec Mimosas.

Kama Simba itawapendeza mnaweza kupata copy ya Pacome pale Asec Mimosas ambapo kuna kijana anaitwa Salifou Diarrasouba.

Kama utakuwa umeifuatilia vizuri Asec Mimosas katika hatua ya makundi ya CAFCL basi utagundua kipaji cha Salifou mwenye umri wa miaka 22. Huyu bwana mdogo ni copy ya Pacome Zouzoua.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMAMOSI