Habari za Michezo leo
Habari za michezo

KUELEKEA MECHI NA MAMELOD….YANGA WAPEWA MTU WA KUMCHUNGA MWANZO MWISHO….

admin March 19, 2024 5:18 pm

Kiungo Mshambuliaji wa Tanzania Prisons, Ally Msengi amesema Yanga ina uwezo wa kushinda mechi za robo fainali dhidi ya Mamelodi Sundowns, lakini akiitahadharisha ihakikishe inakuwa makini na kumbana zaidi straika Peter Shelulile raia wa Namibia.

Yanga imepangwa kukutana na Mamelodi katika mechi za robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika ikianzia nyumbani Machi 30 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam kisha kurudiana ugenini mjini Pretoria Aprili 5.

Hata hivyo, baadhi ya wadau na mashabiki wa soka nchini wameonyesha hofu kwa Yanga ni kupenya kwa wapinzani hao, huku wengine wakiweka matumaini kwa vigogo hao kufanya kweli.

Msengi alisema kwa mfumo wanaoucheza Mamelodi hautofautiani sana na Yanga ya sasa, hivyo iwapo watakuwa makini kudhibiti mipira ya kasi ya wapinzani watatoboa. Alisema Mamelodi wamekuwa na mipira ya kasi na wakiwa nyumbani hupenda kumiliki na kutawala mpira huku wakimtegemea straika wao, Shelulile kufunga mabao.

“Mamelodi wanafungika, nilikutana nao mechi yangu ya kwanza nikiwa na Moroka, wanapenda ile mipira ya kasi na haraka, ukipoteza mpira wakaukamata kasi yao ni kali.”

“Ila Yanga ya sasa wanavyocheza nawapa nafasi ya kushinda mechi hiyo, kikubwa mabeki wawe makini eneo lao kutoruhusu mashambulizi yoyote,” alisema Msengi.

KUELEKEA MECHI NA AL AHLY…ROBERTINHO AMWAGA ‘UPUPU SIMBA’….’BALEKE ANGEWASAIDIA’…. HIVI NDIVYO DUBE ANAVYOZIGONGANISHA SIMBA NA YANGA…ISHU YAKE YAPAMBA MOTO…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply