FT:- AZAM FC 2-1 YANGA
Azam FC

SIKU CHACHE BAADA YA KUILIZA YANGA…MAYELE AMPONGEZA FEI TOTO KWA KAZI NZURI….

admin March 20, 2024 4:48 pm

MSHAMBULIAJI wa zamani wa Yanga SC, Fiston Mayele amempongeza kiungo wa Azam FC ambaye naye amewahi kukipiga Yanga, Feisal Salum ‘Fei Toto’ baada ya kufunga goli la ushindi wa 2-1 kwenye mchezo dhidi ya waajiri wake wa zamani.

Feisal aliibuka Azam FC akitokea Yanga walipokutana kwenye mchezo wa mzunguko wa pili wa ligi uliochezwa Machi 17, 2024 alipachika bao la ushindi dakika ya 52.

Mayele ambaye kwa sasa anaekipiga kwenye klabu ya Pyramid Misri, amempongeza Fei Toto kupitia kwenye post ambayo Feisal aliipost kwenye ukurasa wake inayoonyesha goli alilofunga kwenye mchezo huo na Mayele aliacha comment fupi “Hongera bro”.

Huu unakuwa mchezo wa tatu kwa Feisal kukutana na Yanga toka ajiunge na Azam FC na linakuwa goli lake la kwanza kuiwamba Yanga toka aondoke kwenye viunga vya twiga na Jangwani.

HAWA NDIO MAMELOD AISEEE….YANGA WAKICHOMOKA HAPA WAPEWE TU KOMBE LAO….. KUELEKEA MECHI vs AL AHLY…SIMBA WAMTUPIA ‘MSALA’ WOTE BENCHIKHA….

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply