Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI ZA ROBO FAINAL…SIMBA WAIKIMBIZA YANGA CAF…TAKWIMU HIZI HAPA….

KUELEKEA MECHI ZA ROBO FAINAL…SIMBA WAIKIMBIZA YANGA CAF…TAKWIMU HIZI HAPA….

Habari za Michezo leo

Kwa mara ya kwanza, Tanzania msimu huu imeingiza timu mbili kwenye hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya Simba na Yanga kufika hapo, na sasa zinasubiri kupangiwa wapinzani.

Hata hivyo, kuna wachezaji wa Simba na Yanga ambao ni mara ya kwanza kufika hatua hiyo na hapo Simba imeipiga bao Yanga kwani mastaa wengi wa kikosi cha Wekundu wa Msimbazi tayari wamewahi kufika hatua hiyo.

Katika kikosi cha sasa cha Simba chenye wachezaji 29, ni nyota 12 pekee ambao ni mara ya kwanza kufika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika huku kwa Yanga yenye mastaa 27, wachezaji 25 wamefika hatua hiyo kwa mara ya kwanza.

Kwa Yanga, makipa Djigui Diarra, Metacha Mnata na Aboutwalib Mshery; mabeki Dickson Job, Bakari Mwamnyeto, Nickson Kibabage, Kibwana Shomari, Gift Freddy, Ibrahim Abdallah ‘Bacca’, Joyce Lomalisa na Koassi Attohoula wote ni mara ya kwanza kufika robo fainali ya Ligi ya M abingwa Afrika.

Wengine ni viungo Salumu Abubakar, Zawadi Mauya, Kharid Aucho, Maxi Nzengeli, Pacome Zouzoua, Stephen Aziz Ki, Mudathir Yahya, Shekhan Ibrahim, Farid Mussa, Denis Nkane na Skudu Makudubela huku washambuliaji wakiwa ni Joseph Guede, Clement Mzize na Kennedy Musonda

Hata hivyo, viungo Jonas Mkude na Agustino Okrah ni wachezaji pekee wa Yanga waliofika hatua hiyo na wote walifanya hivyo wakiwa na Simba ambapo Okrah ilikuwa msimu uliopita huku Mkude akiingia mara tatu na Simba.

Kwa upande wa Simba makipa ni Ayoub Lakred na Hussein Abel; mabeki Che Malone Fondoh, Hussein Bakari ‘Kazi’, ilhali viungo ni Babacar Sarr, Abdallah Ismail, Ladack Chasambi, Edwin Balua, Saleh Karabaka na washambuliaji wapo Pa Omar Jobe, Freddy Michael na Willy Onana ndio mara ya kwanza kufika hatua hiyo.

Wengine 17 waliosalia kikosini hapo tayari wamefika katika hatua hiyo na 16 wakiwa na Simba, huku Fabrice Ngoma akifika mwaka 2022 akiwa na Raja Casablanca ya Morocco.

Akizungumzia kufika hatua hiyo kwa mara ya kwanza kiungo wa Simba, Chasambi amesema ni furaha kwake kwa kuwa ni miongoni mwa ndoto zake kufika mbali kwenye ngazi ya klabu.

“Nafurahi kufika hapa. Nashukuru kwa hilo pia nimefurahi. Natamani kufika mbali zaidi na naendelea kulifanyia kazi,” amesema Chasambi.

Kwa upande wa Dickson Job wa Yanga, amesema timu bora ndiyo imechangia wao kufika hapo.

“Yanga kwa sasa tuko vizuri. Tuna timu bora yenye maelewano na ari ya kujituma zaidi. Hiyo ndiyo siri ya sisi kufika hapa,” amesema Job.

Simba na Yanga zinasubiri kujua zitakutana na timu zipi kwenye hatua ya mtoano ya robo fainali ambapo Yanga itakutana na timu moja kati ya Mamelodi Sundowns, Asec Momosas na Petro de Luanda huku Simba itakutana na moja kati ya Al Ahly, Mamelodi na Petro de Luanda.

SOMA NA HII  BAADA YA KUGUNDUA HUENDA MAMBO YAKAENDA KOMBO..PABLO KAAMUA KUJA NA HILI JIPYA MSIMBAZI...