Kwa mara ya kwanza Mwamuzi wa kati aliyechezesha mechi ya juzi kati ya Mamelodi Sundowns na Yanga Beida Dahane raia wa Mauritania amefunguka kwamba asilaumiwe kwa lolote lile kwenye sakata la goli la Aziz Ki kukataliwa bali lawama zote ziwaendee waliokuwa wana-control Video Assistant Referee (VAR)
Mwamuzi huyo ameeleza hayo wakati aki-chat Instagram na aliyekuwa Msemaji wa Klabu ya Yanga,Haji Sunday Manara.
Mwamuzi Beida Dahane ameweka wazi kuwa wakati wa faulo ya @lomalisa4 wanao-control VAR walishindwa kutoa maamuzi hivyo walihitaji msaada wake ndio maana alienda kuwasaidia lakini Kwenye Goli la aziz.ki.10 hakwenda kuthibitisha kwenye VAR kwa sababu haikuwa kazi ngumu kwa wanao-control VAR kutoa maamuzi, walimueleza mapema kuwa sio goli, hivyo kama kuna makosa yoyote walaumiwe wao.
Mwamuzi Beida Dahane @dahane_23 amefunguka kuwa hawezi kuomba msamaha kwa Watanzania kwani hakuhusika katika maamuzi, kama kuna kosa lolote amefanya basi ataomba msamaha kwa Mungu.
Mwamuzi Beida Dahane amesisitiza kwamba yeye ndiyo anatakiwa kuombwa msamaha maana anashambuliwa sana kutokana na sakata hili, wakati wanaotakiwa kushambuliwa ni watu wa VAR.
Aidha pia Beida ameomba radhi kwa tukio hilo, huku akitaka watu wasimshambulie kwa kuwa hakuwa muhusika wa moja kwa moja wa maamuzi ya kukataa goli la Azizi Ki.
Mashuja pongezi kwenu