Home Habari za michezo BENCHIKHA:- UKIACHANA NA YANGA…TANZANIA NZIMA INASHIDA YA WASHAMBULIAJI…

BENCHIKHA:- UKIACHANA NA YANGA…TANZANIA NZIMA INASHIDA YA WASHAMBULIAJI…

Habari za Simba leo

KOCHA Mkuu wa Simba, Abdelhak Benchikha amefunguka na kusema amegundua tatizo la kumalizia (ushambuliaji ) ni janga la nchini kwa sasa kulingana na alivyoona timu nyingi katika Ligi Kuu Tanzania Bara .

Amesema kazi kubwa ni kuhakikisha anaendelea kuwapa mbinu wachezaji wake kuelekea mechi zilizosalia ikiwemo mchezo wa Kariakoo Derby dhidi ya Yanga utakaochezwa jumamosi hii.

Kikosi cha Simba kipo Visiwani Zanzibar kwa ajili ya kambi kujiandaa kwa mchezo huo wa Derby utakaopigwa Jumamosi hii uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam, saa 11:00 jioni.

Kocha Benchikha amesema shida kubwa ya timu yake ni eneo la umaliziaji hilo halipo kwenye timu yake ni sehemu kubwa ya ligi ya Tanzania lakini anahitaji kuendelea kujipanga kuhakikisha washambuliaji wake wanakuwa makini kwenye nafasi wanazotengeneza.

Amesema anaimani kubwa mabadiliko kwa sababu ya mbinu anazowapa katika mazoezi ikiwemo suala la kuwa makini ya kutumia nafasi hizo na kuweza kufunga.

“Hii ni tatizo sio kwetu bali ni asilimia kubwa za timu, lakini naangalia zaidi timu yangu kuna nafasi nyingi tunazotengeneza tunashindwa kufunga, tunakuwa makini na hili kwa sasa ni kukaa na wachezaji kuwaeleza kuwa watulivu katika maeneo,” alisema Benchikha.

Aliongeza kuwa anaimani baada ya msimu huu kufikia tamati atafanyia kazi jambo hilo kwa kuhakikisha wanafanikiwa kuimarisha safu ya ushambuliaji kwa kuweza kutumia nafasi zinazopatikana.

Kocha huyo alisema mechi zijazo watafanya vizuri kwa kutafuta ushindi kwa kila mechi ikiwemo mechi ijayo dhidi ya Yanga ili kuendelea kujiweka katika mazuri ya mbio za ubingwa wa ligi hiyo.

SOMA NA HII  SALEH JEMBE AKAZIA HUKUMU YA TFF KWA MANARA...ADAI MARAFIKI WANAFKI WANAMJAZA UPEPO KUWA HANA MAKOSA...