Habari za Yanga leo
Habari za michezo

ALLY KAMWE:- TUNA OFA KWA AZIZI KI KUTOKA AFRIKA KUSINI, MOROCCO NA MISRI….

admin April 21, 2024 3:25 pm

Meneja Habari na Mawasiliano wa Yanga, Ali Kamwe amesema mpaka sasa klabu hiyo imeshapokea ofa za wachezaji watano kutakiwa na klabu mbalimbali za barani Afrika na Asia, ikiwemo uhitaji wa Aziz Ki.

Akizungumza na HabariLEO, Kamwe amesema Aziz Ki ofa zake zimekuwa zikijirudia “Mtu kama Aziz ofa zake zinajirudiarudia tu, leo utakisikia kutoka South Afrika, kesho Morocco, kesho ofa Misri zinajirudia tu.”

Kamwe amesema baada ya ofa hizo kinachofuata ni kuzijadili kwenye uongozi kuona kama kuna uwezekano wa kuruhusiwa au kubaki nao, amesema wameshazungumza na baadhi ya wachezaji mambo yanaenda vizuri.

Pia Kamwe amegusia tetesi za Mzize kutakiwa na Azam FC, ambapo hakuthibitisha ila amesema alizungumza na Mzize na kumpa mawili matatu. –

Hata hivyo Mzize inafahamika kuwa kashasaini mkataba mpya wa kuendelea kukipiga Yanga kwa muda wa miaka 2 zaidi.

TETESI:- JOBE, FREDDY KUPEWA ‘THANK YOU’ SIMBA…MASTAA WENGINE HAWA HAPA… PAMOJA NA KUFUNGWA JANA….UGONJWA WA SIMBA UKO PALE PALE…..