Habari za Yanga leo
Habari za michezo

KUHUSU HATMA YA UWANJA WA YANGA ENEO LA JANGWANI….ENG HERSI KAJA NA HILI JIPYA…

admin April 30, 2024 7:03 pm

Rais wa Young Africans SC, Eng. Hersi Said, amefichua kwamba, ujenzi wa uwanja wa Klabu hiyo uliopo Makao Makuu ya Klabu, Jangwani, utaanza muda wowote kuanzia sasa.

Eng. Hersi amebainisha kwamba, kinachosubiriwa kwa sasa ni majibu ya barua ya mwisho ya uongozi iliyotumwa kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mohamed Mchengerwa, ikijibiwa na kupatika ardhi yetu, kazi inaanza haraka.

“Tumefanya taratibu zote na barua tumeituma ipo kwa mheshimiwa Mchengerwa ambaye anasimamia Wizara ya Tamisemi na kupitia hapo kuna Tarura waliopewa mradi wa pale Jangwani.

“Baada ya hapo tukishapewa ardhi yetu, Ghalib Said Mohamed (GSM) alionesha nia ya kuwa mmoja wa washirika wa ujenzi wa uwanja na maandalizi upande wake yameshakamilika, tunachosubiri ni kuruhusiwa na Serikali kupitia wizara kupewa ardhi hiyo.

“Niwaambie tu kwamba, siku ambayo tukipata majibu ya barua hiyo ya mwisho, siku inayofuata tutaanza ujenzi,” alisema Eng. Hersi.

DUH!!! HII SASA KALI RAIS YANGA AWAPIGA DONGO SIMBA…”UNATIMUA WACHEZAJI KWA HISIA TU BAADA YA BENCHIKHA KUSEPA ZAKE SIMBA …MAPYA YAIBUKA….ALIKUWA ANALIPWA MIL 50 KWA MWEZI…