Kwa mujibu wa almachiuskanyasi Klabu ya Young Sports Club ilikwishaanza Mazungumzo ya kuwaongezea Kandarasi baadhi inatamatika na wanahitajika klabuni Wachezaji hao ambao Mikataba yao.
Farid Mussa – Ni kweli mkataba wake unatamatika mwishoni mwa msimu huu ila mpaka muda huu hakuna mazungimumzo yoyote yaliyoanza.
Zawadi Mauya – Kweli mkataba wake unatamatika mwishoni mwa msimu huu ila imefahamika kuwa Klabu ya Yanga haina Mpango wa kuendelea kuwa nae.
Denis Nkane – Mwisho wa Msimu huu atakuwa Mchezaji huru na imefahamika kuwa klab yake ya Yanga haina Mpango nae Lena.
Nickson Kibabage – Yes ameshaongeza mkataba mpya wa Miaka 3 baada ya ule wa Mkopo kutamatika.
Clement Mzize – Mkataba wake na Young Africans ulikuwa unaelekea ukingoni ila tayari ameshaongeza kandarasi ya miaka 2.
Makudubela Skudu -Ameshataarifiwa kuwa klab ya Yanga hakina Mpango nae kuelekea Msimu ujao.
Kibwana Shomari – Kweli Mkataba wake na Yanga unaelekea ukingoni ila Mazungumzo ya Mkataba mpya yameanza na klab yake
licha ya kuwa tayari aria ofa 3 mkononi mwake.
Bakar Mwamnyeto – Mazungumzo ya mkataba mpya yameanza na muelekeo wake mzuri, tayari alikuwa na ofa za vilabu viwili vikimuhitaji.
Joyce Lomalisa – Ni kweli Mkataba wake unaelekea tamati na hakuna mazungumzo yoyote ya kuongeza kandarasi Mpya mpaka muda huu.
Metacha Mnata – Kandarasi yake na Klabu ya Yanga inaelekea mwishoni kabisa ila bado hakuna mazungumzo ya mkataba mpya.
Pacome Zouzoua – Ni kweli amesaliwa na mkataba wa mwaka mmoja ila klabu yake imepanga kumuongezea miaka miwili zaidi.
Aziz Ki – Mkataba wake ukiwa ukingoni taarifa za ndani ya uongozi wa Yanga zinadai alishaongeza kandarasi na waajiri wake ambao ni Yanga.
Kuna uwezekano kuna wachezaji Wazawa wasiopungua 3 wataachwa baada ya mikataba yao kuisha na wapo wakigeni pia wasiopungua 4 ili kupisha maingizo mapya.
lmefahamika kuwa Klabu ya Yanga itasajili wachezaji wasiopungua 4 wakigeni, washambuliaji wawli, kiungo mmoja na Mlinzi wa kushoto 1 hao ndio wanawanchi kuelekea dirisha kubwa la usajili.