Home Habari za michezo AHMED ALLY:- KWA UBORA WA SASA TULIONAO SIMBA…UBINGWA WA LIGI NI HALALI...

AHMED ALLY:- KWA UBORA WA SASA TULIONAO SIMBA…UBINGWA WA LIGI NI HALALI YETU…

Habari za Simba leo

Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally amefunguka mara baada ya kushinda bao 3-0 mchezo wao wa Ligi dhidi ya Azam FC na kusema bado wanaitafuta nafasi ya kwanza.

Katika msimamo wa Ligi, Yanga wanaongoza wakiwa na alama 68 katika michezo 25, Azam nafasi ya pili alama 57 na michezo 26 huku Simba wakiwa nafasi ya tatu na alama 56.

“Bado alama moja na safari yetu bado inaendelea, tunaitafuta nafasi ya kwanza. Kwa mujibu wa gepu lililopo, nafasi bado tunayo, sisi hatutafuti nafasi ya pili. Ikitokea tumekwama tukaangukia nafasi ya pili basi hakuna mashaka lakini malengo yetu nasema leo hii ni kuitafuta nafasi ya kwanza.

“Kwa ubora tulionao, tunaiona nafasi ya kwanza inanukia na sisi Simba hatukati tamaa mpaka nafasi ya mwisho. Nilisema Simba itapiganiwa na ambao wana moyo wa kuipigania Simba sio wa kukata tamaa. Kwa wakati ambao watu wanatukatia tamaa, Simba inaanza kushinda mechi zote.

“Tunachokitaka ni kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika, lakini kushiriki Kombe la Shirikisho ni kujidhulumu nafsi zetu na Simba yenyewe, hatuko tayari kwa hilo,” amesema Ahmed.

Mchezo unaofuata wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa timu ya Simba Sc ni dhidi ya Kagera Sugar FC unaotarajiwa kuchezwa siku ya Jumapili ya Mei 12, 2024.

SOMA NA HII  ILI KUTOBOA MICHUANO YA CAF ...GEITA GOLD WAJAZWA UPEPO...WAKIZINGATIA WATALAMBA ASALI KAMA SIMBA ...