Mazungumzo kati ya Menejiment ya Kiungo Fundi Jonas Mkude na klabu ya Yanga yamefikia hatua za mwisho ili mchezaji huyo aweze kusaini kandarasi mpya kuelekea msimu ujao.
Jonas Mkude kuendelea kuwatumikia Wananchi ni pendekezo la Kocha Mkuu Miguel Gamondi kwa Uongozi wa klabu ya Yanga, inatajwa baada ya kumalizika msimu huu ndipo atasaini kandarasi mpya ya mwaka mmoja.
Jonas Mkude ambaye alisaini Yanga mwanzoni mwa msimu huu kwa mkataba wa mwaka mmoja, mpaka sasa hajasaini karatasi zozote za kimkataba.
Katika hatua nyingine, Tovuti ya FarPost kutoka Afrika Kusini imethibitisha kwamba Skudu Makudubela tayari amepokea Ofa kutoka katika Klabu ya Magesi FC ambayo imefuzu kushiriki Ligi Kuu ya Afrika Kusini msimu ujao.
Young Africans SC haina mpango wa kuendelea na huduma ya Kiungo huyu mwenye ustadi wa kuchezea Mpira hivyo ataondoka mwishoni mwa Msimu huu akiwa mchezaji huru.