Home Habari za Yanga Leo JONAS MKUDE ANOGESHA MAZOEZI YA YANGA Z’BAR

JONAS MKUDE ANOGESHA MAZOEZI YA YANGA Z’BAR

Jonas Mkude

Mazoezi ya Yanga yameoga sana! ambapo Jonas Mkude, ni miongoni mwa nyota wa Yanga wanaofanya mazoezi kuelekea fainali ya Kombe la Shirikisho (FA) dhidi ya Azam.

Mcheezo huo umepangwa kuchezwa Jumapili hii kwenye Uwanja wa New Amaan Complex visiwani Zanzibar, ikiwa ni mara ya kwanza kwa fainal hizo kupigwa katika ardhi  hiyo tangu kuanzishwa kwake mwaka 1967.

Kiungo Jonas Mkude alikosekana ndani ya kikosi cha wananchi kwa muda wa takribani wiki mbili baada ya kutokuwa vizuri kiafya.

Aidha kwa upand wa Daktari wa Yanga, Moses Etutu, alisema wachezaji wote wa Yanga SC wanafanya mazoezi baada ya kikosi hicho kufika Zanzibar.

“Kwa ujumla wachezaji wote hali zao kiafya ni wazima, tumekuwa na wachezaji wawili mpaka wanne ambao walikuwa na shida kidogo kama kuumwa malaria na homa akiwemo Jonas Mkude lakini wameanza mazoezi vizuri,” alisema Etutu na kuongeza.

“Hali ya hewa hapa ni upepo na kibaridi kidogo kulinganisha na Dar es Salaam, lakini sidhani kama hali hii itabadilisha mabadiliko ya kimwili kwa wachezaji, pengine inaweza kutusaidia kupunguza uchovu na kuwafanya wachezaji wasichoke mapema, hivyo ni hali ya hewa nzuri na haina madhara kwa wachezaji.”

Klabu ya Yanga inausaka ubingwa wa nane (8) wa Kombe la Shikirikisho la CRDB, ambapo inakuwa ni klabu ya kwanza Tanzania kuongoza kwa kutwaa kombe hilo.

SOMA NA HII  BEKI KISIKI WA SIMBA APIGWA STOP KONGO