Habari za Yanga Leo
MIGUEEL GAMONDI ANAONDOKA YANGA…NAHITAJI KUPUMZIKA NA FAMILIA
Abubakar
June 4, 2024
10:19 am
KOCHA MKUU wa Yanga Miguel Gamondi amesema kwamba baada ya msimu kumalizika akiwa na mafanikio makubwa na kalbu hiyo, anahitaji kuondoka Yanga.
Gamondi alifunguka kila kitu, baada ya mchezo wa fainali wa Kombe la Shirikisho ambapo Yanga walitwaa taji lao la tatu mfululizo.
“Msimu ulikuwa ni mrefu na mgumu. Nahitaji kwenda kupumzika sasa. Nina furaha tumeshinda mataji makubwa, la Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho”
“Naamini hata wazazi wangu mawinguni watakuwa wamefurahi kwa nilichofanya. Nataka kwenda kupumzika sasa nimeimisi familia yangu,”
Msimu uliomalizika kwa Gamondi na Yanga walikuwa na mafanikio makubwa, ubingwa wa Ligi Kuu mara 3 mfululizo na taji hilo kuwa la 30 kwenye historia ya Yanga.
Ubingwa wa 8 wa Kombe la Shirikisho la CRDB, ukiwa ni ubingwa wa 3 mfululizo na wa 4 tangu mashindano hayo yarejee tena mwaka 2015.
Pia kipigo kizito kwa vilabu vyaa Ligi kuu na nje ya Ligi Kuu, Simba ilifungwa goli 7, mzunguko wa kwanza bao 1-5, mzunguko wa pili 2-1.
5G zilikuwa za kutosha na timu zilizoingia kizembe walikutana na msumari wa moto kutoka kwa wananchi, na habari za Yanga leo kutwaa ubingwa wa FA zinazidi kufanya vizuri mitandaoni na duniani kote.
Kufika hatua ya makundi kwa mara ya kwanza baada ya kukaa miaka 25, bila kunusa hatua hiyo Ligi ya Mabingwa Afrika, na walifika hadi hatua ya robo fainali.