Home Habari za michezo SIMBA NA YANGA KUPIGWA MARA 3…MSIMU WA 2024/25

SIMBA NA YANGA KUPIGWA MARA 3…MSIMU WA 2024/25

Simba na Yanga

HUENDA SIMBA NA YANGA zikikakutana zaidi ya mara 3 kwa msimu ujao wa mashindano, 2023/24, lakini kwa kufuata Kanuni za Ligi timu tutashuhudia Dabi ya Kariakoo mara 3 kuanzia mechi za Ngao ya Jamii.

Kwa mujibu wa kanuni za ligi, mechi za nusu fainali ya Ngao ya Jamii, inashirikisha timu nne na mshindi wa kwanza wa ligi msimu uliomalizika anakutana na mshindi wa tatu.

“Shindano maalum la ufunguzi wa Ligi (Ngao ya Jamii) litashirikisha timu zilizoshika nafasi tatu za juu kwenye msimamo wa Ligi na Timu Bingwa wa Kombe la Shirikisho”.

“Endapo Bingwa wa Kombe la Shirikisho atakuwa miongoni mwa washindi wa nafasi tatu za juu kwenye msimamo wa Ligi Kuu, timu iliyoshika nafasi ya nne katika msimamo wa ligi itashiriki shindano hilo”.

“Hatua ya Nusu Fainali itakuwa na michezo miwili, mchezo wa kwanza utakaoshirikisha bingwa wa Ligi Kuu dhidi ya timu iliyoshika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu.

“Mchezo wa pili utashirikisha timu iliyoshika nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu dhidi ya bingwa wa Kombe la Shirikisho/timu iliyoshika nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu,”

Inafafanua kanuni ya 19 ibara ya pili ya ligi kuu kwa kuzingatia msimu uliomalizika.

Kutokana na hilo, Azam ambayo imeshika nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu, itamenyana na Coastal Union ambayo imemaliza msimu ikiwa nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi.

Uhakika wa Simba na Yanga kukutana mara tatu msimu ujao, ni muendelezo wa timu hizo kukutana mara nyingi ndani ya msimu mmoja tofauti na miaka ya nyuma ambapo zilikuwa zikikutana mara mbili tu ikiwa ni kwenye Ligi Kuu.

Msimu uliopita, timu hizo zilikutana mara tatu ambapo moja ilikuwa ni kwenye fainali ya Ngao ya Jamii mkoani Tanga kwenye Uwanja wa Mkwakwani ambapo Simba ilipata ushindi na mara mbili kwenye Ligi katika Uwanja wa Benjamin Mkapa ambapo Yanga iliibuka mbabe kwenye mechi zote.

Timu hizo zilikutana mara nne katika msimu wa 2022/2023, mbili kwenye Ligi na moja katika Ngao ya Jamii ambapo kila timu ilipata ushindi mara moja na matokeo ya sare yalikuwa kwenye mchezo mmoja.

Mara nne tofauti, timu hizo zilikutana katika msimu wa 2021/2022 ambapo Yanga iliibuka na ushindi mara mbili na zilitoka sare mara mbili.

Msimu wa 2020/2021, timu hizo zilikutana mara tatu ambapo Simba ilipata ushindi mara moja na zilitoka sare moja.

Katika msimu ujao, timu hizo zinaweza kukutana zaidi ya mara tatu ikiwa kila moja itafanya vyema kwenye mashindano tofauti inayoshiriki.

Ukiondoa Ngao ya Jamii na Ligi Kuu, zinaweza pia kukutana kwenye Kombe la Shirikisho la CRDB ambalo linachezwa kwa mtindo wa mtoano lakini pia zinaweza kuumana kwenye Kombe la Mapinduzi na pia Kombe la Muungano.

SOMA NA HII  DILUNGA HUMWAMBII KITU KWA CHAMA.