Habari za Simba Leo
STEVE KOMPHELA WA MAMELODI…FILE LAKE LINAJADILIWA SIMBA
Abubakar
June 5, 2024
10:21 am
UNAIKUMBUKA Mamelodi Sundowns ya Pitso Mosimane? huenda huko mbali, je hii Mamelodi ya Rulani Mokwena? kwenye ubora ule na kiwango kile nyuma yake alikuwepo Kocha Steve Komphela ambaye jina lake lipo kwenye meza ya Mnyama Simba likiendelea kujadiliwa.
Inaelezwa kwamba Steve Komphela ambaye kwa sasa anafundisha klabu ya Golden Arrows inayoshiriki Ligi kuu ya Afrika Kusini, anatajwa kuwa Mrithi wa nafasi ya Benchika ambayo ilikuwa ikikaimiwa na Juma Mgunda.
Simba na Coastal Union wamemalizana na Kocha Mgunda ambaye, atajiunga nao kama kocha mkuu ili kukinoa kikosi hicho cha Wagosi wa Kaya kwenye mashindano ya kimataifa ya Kombe la Shirikisho, ratiba inaonesha Agosti michuano hiyo itaanza kwa timu zinazoanzia hatua ya awali kabisa.
CV YA KOCHA HUYU USIPIME
Wasifu wa Kocha huyu ambaye amefundisha kama kocha mkuu wa Mamelodi na kocha msaidizi chini ya makocha wakubwa kama Pitso na Mokwena, nadhani imewavutia zaidi Simba hadi kufikia hatua ya kumtaka haraka. Ni muumini wa mfumo wa 4-4-2 double 6.
2023/24: Amefundisha kama kocha Mkuu Golden Arrows.
2023/24 (Julai4- Feb 19-2024): Moroka Swallows
Oktoba 24, 2022/23: Mamelodi Sundowns- (Kocha Msaidizi)
2020/21: Mamelodi Sundowns, Kocha Mkuu.
2018/19: Golden Arrows, Kocha Mkuu.
2017/18: B.Fontein Celtic, Kocha Mkuu
2015/16: Kaizer Chief, Kocha Mkuu
2013/14: Maritzburg Utd, Kocha Mkuu
2011/12, Timu ya Taifa ya Afrika Kusini, Kocha Msaidizi.
Pia kocha huyo, kwa wakati tofati amewahi kuwa kocha Mkuu wa vilabu kama, FS Stars, Platnum Stars, Afrika ya Kusini chini ya umri wa miaka 20, Dynamos FC na Maning Rangers.