Home Habari za michezo KUHUSU PACOME KUTAKIWA AL AHLY….YANGA WAMEIBUKA NA TAARIFA HII MPYA…

KUHUSU PACOME KUTAKIWA AL AHLY….YANGA WAMEIBUKA NA TAARIFA HII MPYA…

Habari za Yanga

OFISA wa habari wa Yanga, Ally amepunguza taharuki baada ya kuwepo kwa taarifa juu ya kiungo wao Pacome Zouzoua kuwa yupo sokoni baada ya Al Ahly kuweka dau.

Taarifa hiyo imezua taharuki kwa mashabiki wa klabu hiyo kwa kuhofia kiungo huyo kuondoka ndani ya kikosi cha timu hiyo hali ya kuwa msimu uliopita ameonyesha uwezo mkubwa.

Baada ya taharuki hiyo kwa mashabiki, Ofisa habari wa Yanga, Ali Kamwe ametoa tahadhari kuwa nyota huyo hauzwi na wapo kwenye mazungumzo ya kumuongeza mkataba.

“Huo ni uzushi na uongo kuwa Pacome anaondoka Yanga, hakuna ofa iliyofika mezani kwetu, tulikuwa na mkataba wa mwaka mmoja na mazungumzo yanafanyika kuongeza mwingine kusalia ndani ya kikosi,” amesema Kamwe.

Ameongeza kuwa jitihada kubwa inaendelea kufanyika kwa sababu malengo yao ni kucheza nusu na fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

“Hatufikirii kuacha mchezaji yoyote aliyekuwa kwenye mipango ya kocha Gamond akiwemo Pacome yupo kwenye mikakati yetu kuelekea msimu ujao wa mashindano,” amesema Ofisa huyo.

Kamwe amesema wananchi wanatakiwa kutulia na kuwa wavumilivu kwa kipindi hiki ambacho wapo kwenye mchakato wa usajili wa wachezaji wapya na wanaongezwa mkataba.

SOMA NA HII  SIMBA KWELI NI BABA LAO...BODI YA LIGI YABADILI RATIBA KISA CAF...YANGA KAMA KAWA...