Home Habari za michezo BAADA YA CHAMA KUSEPEA ZAKE YANGA….HII HAPA MASHINE INAYOKUJA KUMRITHI SIMBA…

BAADA YA CHAMA KUSEPEA ZAKE YANGA….HII HAPA MASHINE INAYOKUJA KUMRITHI SIMBA…

Tetesi za Usajili Simba

Klabu ya Simba inatajwa kukamilisha usajili wa kiungo kutoka Jamhuri ya Congo Debora Mavambo Fernandesn aliyekuwa aakiitumikia Mutondo Stars ya Ligi Kuu Zambia (MTN).

Kiungo huyo wa kati mzaliwa wa Angola mwenye umri wa miaka 24 tayari yuko nchini na huenda akawa miongoni mwa wachezaji watakaotambulishwa na Simba siku chache zijazo.

Debora ameitumikia Mutondo FC msimu mmoja akijiunga akitokea klabu ya Academica Petroleos do Lobito ya Angola mwaka 2023

Kiungo huyo anamudu kucheza eneo la kiungo mkabaji lakini pia mara chache ametumika katika safu ya ulinzi. Ujio wa Debora huenda ukashuhudia Simba ikiachana na Sadio Kanoute au Babacar Sarr.

Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Ahmed Ali amesema uongozi uko kwenye majadiliano ya kusitisha mikataba ya baadhi ya wachezaji. Taarifa za wachezaji hao kupewa ‘Thank You’ zitatolewa baada ya michakato hiyo kumalizika.

Miongoni mwa majina makubwa watakopewa ‘Thank You’ ni pamoja na Clatous Chama ambaye hivi leo ametambulishwa Yanga kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Wengine waliopigwa panga Simba ni pamoja na Luis Jose Miquissone, Kennedy Juma, John Bocco, Saido Ntibazonkiza, Chillunda na Musa Mohammed.

SOMA NA HII  PAMOJA NA KUANZA VYEMA SIMBA...PABLO ASHINDWA KUJIZUIA..AFUNGUKA MSIMAMO WAKE...