Home Habari za michezo CHAMA AHAMIA YANGA NA KIJIJI…..MASHABIKI 3000 WA SIMBA WAHAMA NAYE….

CHAMA AHAMIA YANGA NA KIJIJI…..MASHABIKI 3000 WA SIMBA WAHAMA NAYE….

HABARI ZA YANGA-CHAMA

MSEMAJI wa Klabu ya Yanga, Ali Kamwe amesema mashabiki zaidi ya 3,000 wamehama pamoja na kiungo mpya wa timu hiyo Clatus Chama na kujiunga na Yanga.

Sasa wanaandaa utaratibu wa kuwapokea na kuwatangaza kuwa mashabiki wao wapya ndani ya klabu hiyo.

Kamwe amesema kati ya mashabiki hao waliohamia katika timu hiyo wakimfuata Chama baba yake mzazi ni miongoni mwao ingawa alimtaka asimtangaze kama amehamia Yanga.

β€œBaba yangu amesema kutokana na utu uzima wake, afya na mambo mengine, hayupo tayari kuendelea kujitesa na Simba amehamia Yanga, ameniomba nisimtangaze, mimi nimeshindwa kuvumilia nimemtangaza atakuwa miongoni mwa mashabiki tutakaowatangaza,” amesema.

Yanga wamemtangaza Chama kumsajili mkataba wa mwaka mmoja na klabu hiyo akiwa mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake na Simba.

Kamwe amesema licha ya faida hiyo pia Chama atasaidia Yanga kibiashara, kuanzia jezi na vitu mbalimbali vikiwemo makampuni mbalimbai kujitokeza kuwekeza kwa klabu hiyo.

Mchezaji kufuatwa na mashabiki ni kitu cha kawaida Roanaldo alivyohama kutoka Manchester United kujiunga na Real Madrid alihama na mashabiki wengi walimfuata kutokana na mapenzi ya mashabiki hao kwa Ronaldo, ndivyo ilivyokuwa kwa Chama na baadhi ya mashabiki wake.

SOMA NA HII  FEISAL SALUM LEO MKWAWANI KUNACHIMBIKA , YANGA WAJIPANGE