Home Habari za Usajili Yanga KIMEELEWEKA YANGA…MWAMNYETO KULIPWA MIL 10…MKATABA WAKE MPYA UKO HIVI.

KIMEELEWEKA YANGA…MWAMNYETO KULIPWA MIL 10…MKATABA WAKE MPYA UKO HIVI.

Habari za Yanga

HATIMAYE Iko Wazi, Uongozi wa klabu ya Yanga umethibitisha kumuongeza mkataba wa miaka miwili beki kitasa Bakari Nondo Mwamnyeto, utakaomalizika hadi mwaka 2026.

Mkataba huo wa miaka miwili umefanya nyota huyo avune takribani milioni 300 na mshahara wa takribani milioni 10 Kwa Mujibu wa chanzo Cha ndani kutoka Kwa watu wa karibu wa Beki huyo.

Mwamnyeto ameongeza mkataba huo, baada ya kufikia muafaka mzuri na Uongozi wa timu hiyo, katika dau la usajili na mshahara atakaouchukua ndani ya miaka miwili atakayokuwepo hapo.

Beki huyo alisaini mkataba huo, chini ya Mtendaji wa Klabu ya Yanga, Andre Mtine na Menejimenti ya Mwamnyeto.

Mwamnyeto amekuwa akitengeneza ukuta wa Yanga akishirikiana na mabeki wengine wa kati akiwamo Ibrahim Hamad ‘Bacca’, Dickson Job na Gift Fred, japokuwa mara nyingi alikuwa akianzia benchi kuwapisha wenzake kuanza kikosi cha kwanza.

Kabla ya kutua Yanga mwaka Agosti 2020, Mwamnayeto aliitumikia Coastal kwa misimu miwili akiwa pia kama nahodha akitengeneza ukuta imara kwa kushirikiana na Ibrahim Ame ambaye alisajiliwa na Simba wakati Nondo akitua Yanga.

Awali Bakari Mwamnyeto alikuwa anahusishwa zaidi kujiunga na Simba, ambao walikuwa wakimfuatilia mchezaji huyo tangu akiwa Coastal Union, na msimu huu kidogo dili litiki,  lakini Yanga fasta wakashitukia  mchongo.

SOMA NA HII  KUELEKEA KARIAKOO BADI....ALLY KAMWE AWATISHIA 'NYAU' SIMBA....