Home Habari za Simba Leo COASTAL UNION YAZIDI KUWEKA MSIMAMO…YAMUITA KAMBINI LAMECK LAWI

COASTAL UNION YAZIDI KUWEKA MSIMAMO…YAMUITA KAMBINI LAMECK LAWI

HABARI ZA SIMBA, LAMECK LAWI

Coastal Union imeendelea kuikazia Simba kwa kumng’ang’ania beki wao wa kati Lameck Lawi, ambaye hapo awali walikubaliana kumuuza kwa Wekundu hao kabla ya kubadili gia hewani.

Lameck Lawi, mwenye mkataba wa mwaka mmoja na Coastal, alishatambulishwa na Simba baada ya kudaiwa kukubaliana na Wagosi pamoja na mchezaji mwenyewe, lakini kitendo cha mabosi wa Msimbazi kuchelewesha fedha kiliwafanya Wana Mangushi kubadili mawazo na sasa wamekazia msimamo huo huo.

Katibu Mkuu wa Coastal, Omary Ayoub alisema, hawana wanachoweza kufanya kwa sasa juu ya Simba kumsajili Lawi na kwamba timu inaendelea na maisha ikiwa na beki huyo anayetajwa ameingia kambini jijini Tanga kujiandaa na michuano ya Kombe la Kagame itakayoanza rasmi Jumanne ijayo.

Ayoub alisema, Lameck Lawi ni mali ya Coastal na anaendelea kujifua akiwa nasi, hivyo watu watamuona beki huyo katika michuano hiyo ya Kagame.

“Mambo ya Simba na Lawi waulizeni wenyewe sisi msimamo wetu uko palepale, huyu ni mchezaji wetu na tunaendelea na maisha yetu kama ilivyokuwa hapo kabla, mjadala huu tulishaufunga,” alisema Ayoub na kuongeza;

“Lawi yupo Coastal anaendelea na kazi kwa mujibu wa mkataba alionao wanaodhani atacheza timu nyingine wasubiri kumuona Julai 9 katika michuano ya Kagame. Amekuwa hapa tangu siku ya kwanza ya mazoezi na yuko timamu na kazi yake, hivi tunavyoongea Lawi ni kati ya wachezaji wanaojiandaa kuja Dar es Salaam.”

Afisa Habari watimu hiyo kwenye kufafanua suala hilo, alisema kuwa mchezaji huyo ataenda kucheza Ulaya nchi ya Ubelgiji.

SOMA NA HII  KISA KUNYUKWA NA SIMBA...MUSONDA ASHINDWA KUAMKA...AMEFUNGUKA HAYA