Home Habari za Yanga Leo IBENGE ATETA NA CHAMA & AZIZ KI…AFICHUA KILICHO MUAONDOA CHAMA BERKANE

IBENGE ATETA NA CHAMA & AZIZ KI…AFICHUA KILICHO MUAONDOA CHAMA BERKANE

HABARI ZA YANGA, CHAMA

Florent Ibenge Kocha mku wa Al Hilal amemzungumzia nyota mpya aliyesajiliwa na Yanga kutoka Simba, Clatous Chama na kilichomkwamisha kufanya vizuri Morocco, huku akitia neno kwa kiungo wa Yanga, Stephane Aziz Ki akisema ni miongoni mwa mastaa anaowakubali sana na kufichua maisha ya Sudan yalivyo.

CHAMA KUONDOKA RS BERKANE

Baada ya kiungo Clatous Chama kufanya vizuri msimu wa 2020/21 akiichezea Simba, uongozi wa RS Berkane ukavutiwa na kiwango chake ukamsajili msimu wa 2021/2022 ambao alidumu kwa miezi sita kisha akarejea tena kwa wana Msimbazi.

Ukimuuliza Chama alifeli wapi, Ibenge ambaye ndiye aliyemsajili Mwamba wa Lusaka pale Berkane, atakujibu: “Chama ni mchezaji mwenye uwezo mkubwa, ana ujuzi, kipaji kikubwa, hakuna kocha ambaye anaweza asitamani kuwa naye kwenye kikosi chake.

“Kitu kilichomrudisha Tanzania ni suala la familia yake, ikumbukwe alipoteza mkewe, aliacha watoto wake Zambia, hivyo alihitaji ukaribu na watoto wake.

“Naheshimu sana familia nilimuelewa alivyosema anahitaji kukaa karibu na watoto wake, kama watoto hawana mama watahitaji kumuona baba yao.”

Kuhusu Tripple C kwenda Yanga, Ibenge anasema: “Kama nilivyosema, Chama ni mchezaji mzuri na kwenda kwake Yanga itakuwa faida kubwa kwa timu hiyo.”

AZIZ KI

Ibenge alizungumza kuhusu kiungo mshambuliaji Aziz Ki, ambaye amemaliza mkataba wake na Yanga mwezi uliopita, kama anavutuwa naye na angependa kumsajili katika kikosi cha timu yake ya Al Hilal.

“Niliwahi kumhitaji wakati anachezea ASEC Memosas, lakini alichagua kwenda Yanga, kiukweli ni mchezaji mzuri na sidhani kama kuna kocha asiyemtamani, ukiwa naye ni jambo zuri katika timu.”

SOMA NA HII  IMEFICHUKA MPANZU AFICHWA HOTELINI NA SIMBA...MO DEWJI AHUSIKA